
RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein, akihutubia Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar kabla yac
kulivunja rasmin leo katika ukumbi wa mkutano Chukwani Jijinin
Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein,
akikabidhiwa zawadi ya Kitabu Maalum cha Miswada ya Sheria na Picha ya
Jengo la Baraza la Wawakilishi Zanzibar, na Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid, baada ya hafla ya kulivunja
rasmin Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar, hafla hiyo imefanyika
katika ukumbi wa Baraza Chukwanin Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

MAKAMU wa
Pili wac Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar. Mhe Said Hassan Said na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, wakifuatilia
hutuba ya uvunjaji wa Baraza la Tisa la Wawakilishi wakati Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein.(hayupo pichani) akihutubia kabla ya kulivunja Baraza leo katika
ukumbi wa Baraza Chukwanin Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

WAJUMBE
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wa kwanza Mhe. Jaku Hashim Ayoub akiwa
na wajumbe wakishangilia wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani)
akihutubia hafla hiyo ya uvunjaji wa Baraza la Wawakilishi uliofanyika
leo katika ukumbi wa mkutano Chukwani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

BAADHI ya
Mabalozi Wadogo Wanaofanyika Kazi zao Zanzibar wakifuatilia hutuba ya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein,(hayupo pichani) akihutubia na kulivunja rasmin Baraza la
Tisa la Wawakilishi Zanzibar, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa
mkutano wa Baraza Chukwani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu).

WAGENI
Waalikwa kutoka Taasisi ya Fedha Zanzibar wakifuatila hutuba ya Uvunjaji
rasman wa Baraza la Tisa la Wawakilishi wakati Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo
pichani) akihutubia na kulivunja rasmin Baraza leo.(Picha na Ikulu).

WAGENI
wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo pichani) akihutubia kab la
ya kulivunja Baraza la Tisa la Wawakilishi.(Picha na Ikulu).

WAKUU wa
Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakifuatila hutuba ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed
Shein.(hayupo pichani) wakati wa hafla ya uvunjaji rasmin wa Baraza la
Tisa la Wawakilishi Zanzibar.(Picha na Ikulu).



******************************
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema Serikali itaendelea
kuhakikisha hali ya amani na utulivu iliopo nchini inaendelea kudumu
kabla na baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Dk. Shein amesema hayo leo katika
Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni , nje kidogo ya Jiji la Zanzibar
wakati akilivunja Baraza la Tisa la Wawakilishi.
Alisema Serikali imetunga sheria
ya Uchaguzi namba 4 ya mwaka 2018, kwa lengo la kuweka utaratibu bora wa
Uchaguzi na kuondoa kasoro zote zilizojitokeza katika chaguzi
zilizopita, hivyo ni wajibu wa Viongozi wa vyama vya siasa na wanachama
kuheshimu, kazi na majukumu ya Tume za Uchaguzi nchini (ZEC na NEC),
akibainisha vyombo hivyo vimeundwa kikatiba.
Alisema hatua yoyote ya kuchukua maamuzi kinyume na utaratibu uliowekwa na sheria, utasababisha zogo na kuanzisha fujo.
“Zogo na fujo ndio chanzo cha watu
kugombana na hatimae kuingiana maungoni, hayo sio madhumuni ya
uchaguzi, kwa hivyo uchaguzi wa Oktoba mwaka huu utakuwa huru na haki”,
alisema.
Alitoa indhari kwa wale wenye nia
ya mawazo ya kutaka kuharibu uchaguzi kwa njia yoyote ile au kufanya
fujo, waondokane na fikra hizo, kwani jambo hilo halitowezekana kwenye
uchaguzi wa mwaka huu.
Aidha, aliwahakikishia wananchi
kuwa sheria za uchaguzi, katiba pamoja na fedha za kuendesha uchaguzi
huo zipo kutoka Serikalini na kubainisha kuwa vikosi vya Ulinzi na
Usalama viko makini kusimamia uchaguzi huo.
“Nawatangazia mimi na Dkt. John
Pombe Joseiph Magufuli tupo macho, hatutasinzia seuze kulala,
tutatekeleza wajibu wetu na watakaofanya vituko dhidi ya sheria
tutawashughulikia”, alisema.
Aidha, Rais Dkt. Shein alisema
Serikali imeamua kuzifungua skuli zote za maandalizi, msingi na
Sekondari Unguja na Pemba kuanzia Jumatatu ya Juni 29, mwaka huu.
Alisema hatua hiyo inatokana na
hali ya ugonjwa wa Corona hivi sasa kuwa shwari kuliko ilivyokuwa mwezi
wa April, Mei na wiki ya mwanzo ya mwezi wa Juni, akibainisha kutowepo
kwa mgonjwa hata mmoja katika vituo vyote vilivyokuwa vikiwatibu
wagonjwa Unguja na Pemba.
Alisema ni muda wa siku kumi umepita tangu mgonjwa wa mwisho kutoka katika vituo hivyo, hali inayobainisha kuwa ni shwari.
Hata hivyo, aliitaka Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya amali kuandaa mipango madhubuti na kabambe ya namna
bora zaidi kwa wanafunzi wanapokuwa masomoni, ikizingatiwa mazingira ya
madarasa mengi kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.
Vile vile, aliutaka uongozi wa
Kampuni za Boti na meli zinazosafiri kati ya Zanzibar na Dar es Salaama
pamoja na Unguja , Pemba na Tanga kuhakikisha zinachukua abiria kwa
mujibu ya viti ya vyombo vyao kama ilivyosajiliwa , kuanzia Juni 29,
mwaka huu.
“Abiria hawataruhusiwa kusimama au
kukaa popote wakiwa safarini, Serikali itachukua hatua dhidi ya Kapteni
na kukifungia chombo chochote kitakachokiuka mashart haya”, alisema.
Aliitaka Wizara ya ujenzi,
Mawasiliano na Usafirishaji, Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA) pamoja na
Shirika la Bandari kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo sambamba na
kuhakiki ‘manifesto’ za wasafiri wote wanaopanda na kushuka ili
kujiridhisha.
Aidha, Dk. Shein aliwataka wafanya
biashara kufanya shughuli zao kwa nidhamu pamoja na kuruhusu shughuli
za kijamii kuendelea kama kawaida; ikiwemo arusi, maulidi, hitma na
kadhalika, huku akiwataka wananchi kuzingatia taratibu na kanuni za Afya
kama inavyoshauriwa na wataalamu ili kuepuka maambukizi, akibainisha
virusi vya Covid 19 kuwa bado havijamalizika kabisa.
Kuhusiana na michezo, Dk. Shein
alisema Serikali imeruhusu kuendelea kwa mchezo ya mpira wa miguu pekee
katika ngazi za Ligi kuu na Premier, na kuwataka wanamichezo mingine
wakiwemo wa riadha pamoja na mazoezi ya viungo kuvuta subira..
Katika hatua nyengine, Dk. Shein
aligusia maendeleo ya kiuchumi nchini katika kipindi cha miaka 10 ya
uongozi wake, na kusema Serikali imeendelea na juhudi za kutekeleza
mipango ya kiuchumi ili kuhakikisha ustawi wa wananchi wa Zanzibar
unaimarika.
Akinukuu vifungu mbali mbali
kutoka Ilani ya Uchaguzi mkuu ya CCM ya mwaka 2010 na mwaka 2015, Dk.
Shein alisema Ilani iliielekeza Serikali kujenga mazingira
yatakayowezesha uchumi wa Zanzibar kufikia kiwango cha uchumi wa nchi
zenye kipato cha kati.
“Ilani ilielekeza kuhakikisha
mfumko wa bei unabaki katika tarakimu moja na wastani wa pato la kila
mwananchi linaongezeka”, alisema.
Aidha, alisema Ilani ilielekeza
mapato yaendelee kudhibitiwa pamoja na kuwepo nidhamu katika matumizi ya
Serikali, kupunguza utegemezi wa wahisani wa maendeleo, misamaha ya
kodi isiyokuwa na tija, sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha
ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Alisema katika kipindi hicho cha
miaka 10, Pato la taifa limeweza kukua kutoka thaamni ya shilingi
Bilioni 1.7 (mwaka 2010) hafi kufikia thamani ya shilingi Bilioni 3,
ikiwa sawa na mara 1.74, zaidi ya wakati Awamu ya saba ikiingia
madarakani.
Alielelza kuwa kasi ya ukuaji uchumi nayo imeongezeka kutoka asilimia 4.3 (2010) hadi kufikia asilimia 7.0 mwaka 2019.
Vile vile, alisema Pato la
mwananchi nalo limeongezeka kutoka shilingi 942,000 (USD675) mwaka 2010
hadi kufikia shilingi 2,549 (USD1,114) mak 2019, ikiwa sawa na asilimia
170.59.
Aidha, alisema mfumko wa bei
ulishuka kutoka asilimia 14.7 (2011) hadi asilimia 2,9 mwaka 2019, na
kubainisha hali hiyo imeleta faraja kubwa kwa wananchi kwani wameweza
kupata bidhaa muhimu kwa bei ya kuridhisha.
Nae, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, akitoa shukuran kwa Rais Dk. Shein
alimtakia afya njema, umri mrefu na mapumziko mema baada ya kulitumikia
Taifa kwa mafanikio makubwa.
Aidha, alimkabidhi Dk. Shein
zawadi za sheria zote 128 zilizopitishwa na Baraza hilo katika kipindi
cha Uongozi wake, pamoja na zawadi ya umbo linalofanana na jengo la
Baraza la wawakilishi, kwa ajili ha kumbukumbu yake.
Hafla hiyo, iliyohudhuriwa na Mke
wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Majaliwa Kasssim Majaliwa, Makamu w aPili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania Job Ndugai pamoja viongozi mbali mbali wa serikali, wastaafu
na baadhi ya mabalozi a nchi za nje.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...