Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inapenda kuwajulisha wananchi kuwa inashiriki maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika Uwanja wa Maonyesho wa Biashara wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 01/07/2020 hadi tarehe 13/07/2020.

Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na mikoa ya jirani mnakaribishwa kutembelea Banda letu lililopo ukumbi wa Karume  ili muweze kupata huduma mbalimbali zinazohusiana na afya ya Moyo.

Madaktari wetu bingwa wa magonjwa ya moyo chini ya uongozi wa Prof. Mohamed Janabi watakuwepo  katika banda letu kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...