Mwanamke Asha Juma, anayeishi Manzese Argentina jijini Dar es Salaam akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.
Mwanamke Asha Juma, anayeishi Manzese Argentina jijini Dar es Salaam akitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo. 

MWANAMKE Asha Juma, anayeishi Manzese Argentina jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka mawili ya kumiliki risasi 45 kinyume Cha Sheria.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Adolph Lema leo Agosti 12, 2020 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Agustina Mmbando imedai  Mei 17, 2020 katika eneo la Manzese jijini Dar es Salaam mshtakiwa Asha alikutwa akimiliki risasi 29 zenye kipenyo milimita 12 kinyume cha sheria ya usimamizi wa silaha na risasi nchini.

Katika shtaka la pili imedaiwa, Siku na mahali hapo Asha alikutwa akimiliki risasi 16 zenye kipenyo cha milimita 9 kinyume na sheria ya usimamizi wa silaha na risasi.

Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu chochote  mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi ambazo kwa kawaida zinasikilizwa Mahakama Kuu au kwa kibali maalimu kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Agosti 26, mwaka huu. Mshtakiwa amerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...