
Mgombea wa Urais ,Prof.Ibrahim
Lipumba akikabidhiwa Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi CUF katika
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 na Mwenyekiti wa Tume
ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi
za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Prof.Ibrahim
Lipumba wakionyesha Begi lenye Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi CUF katika
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 pamoja na Mgombea
Mwenza Bi.Hamida Abdallah mara baada ya kuchukua Fomu hizo katika Ofisi
za Makao Makuu ya NEC Njedengwa leo jijini Dodoma.

Mgombea wa Urais ,Prof.Ibrahim
Lipumba kupitia Chama cha Wananchi CUF katika Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 akisaini Kitabu mara baada ya
kuchukua Fomu hizo za Kugombea Urais katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC
Njedengwa leo jijini Dodoma kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) Dk. Wilson Mahera Charles.




Baadhi ya wafuasi wa chama cha
Wananchi CUF waliomsindikiza Mgombea wa Urais ,Prof.Ibrahim Lipumba
aliyeambatana na Mgombea Mwenza Bi.Hamida Abdallah kwa ajili ya kuwania
nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho
katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 wakiwa
wakifatilia kwa umakini katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa
leo jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...