Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV

MKURUGENZI wa taasisi ya Kumekucha Tanzania inayoshirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Jackson Cyprian ameeleza kushangazwa na baadhi ya viongozi wa mikoa ambao wanasuasua kutoa ushirikiano katika mpango wa Serikali kutokomeza malaria nchini.

Akizungumza leo Agosti 6,2020  jijini Dar es Salaam Cyprian  amesema tangu kampeni ya kutokomeza malaria nchini kupitia maazimio ya mikoa na hasa ikilenga  kutekeleza agizo la Rais John Magufuli alilolitoa Juni 2019 la kutaka Tanzania ijikomboe na ugonjwa wa muda mrefu wa malaria.

Amefafanua pamoja na kuwepo kwa maelelezo hayo ya Rais lakini bado kuna baadhi ya mikoa hasa makatibu tawala kutotoa ushirikiano, hivyo ametoa rai kwa viongozi hao pamoja na wengine kushiriki kikamilifu kwenye mpango huo wa kutokomeza malaria.

"Kumekucha tumepewa dhamana na NDC kuratibu kampeni ya matumizi ya viuadudu ili kuangamiza viluilui vya mbu lakini tumekuwa tukiandika barua na kupiga simu kwa ajili ya kuomba vikao na mikutano ya kutoa maazimio ili tumalize malaria kwenye mikoa husika lakini hatupewi ushirikiano"amesema jackson

Aidha ameipongeza mikoa ya Mbeya na Songwe kwa kuchukua hatua ba hatimaye kuja na azimio la kumaliza malaria katika mikoa yao."Wanastahili kupongezwa mikoa ya Mbeya na Songwe kwa uamuzi huu mzuri."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...