
Mhadhiri Msaidizi wa idara Ustawi wa Jamii taaluma wa Taasisi ya Ustawi wa jamii Rufina Khumbe akitoa elimu kwa akinamama wa Bariadi Mkoani Simiyu waliofika katika dawati la Taasisi ya Ustawi wa Jamii kupata huduma

Kutoka kushoto ndani ya banda, wahadhiri wasaidizi wa idara Ustawi wa Jamii taaluma Rufina Khumbe na Dunstan Haule wa Taasisi ya Ustawi wa jamii wakitoa elimu kuhusu Taasisi ya Ustawi wa Jamii kazi na huduma inazotoa kwa wageni waliofika kupata huduma kwenye banda la Wizara ya Afya –idara kuu ya Maendeleo ya Jamii

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mahaha ya Bariadi mkoani Simiyu wakiwa na nyuso za furaha baada ya kutapa maelezo ya kozi inazotolewa na Taasisi na kujua kuwa wao ni wanafunzi watarajiwa wa elimu ya juu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na kila mmoja wao kupata nakala ya vipeperushi vya Taasisi ya Ustawi wa Jamii vinavyotolewa kwa wateja wote wanaofika katika dawati la huduma
…………………………………………………………………
Taasisi ya Ustawi wa Jamii katika maonesho ya Nane Nane mkoani Simiyu inatoa elimu juu ya masuala ya ustawi wa jamii, jinsia na maendeleo ikizingatia kauli mbiu ya mwaka huu,” KWA MAENDELEO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.
Taasisi inatoa elimu kwa wanajamii wa Simiyu na maeneo yanayopakana na simiyu kuhusu masuala ya kijamii, wanawake na watoto. Vilevile, Taasisi imejikita katika kutoa elimu juu ya jinsia na maendeleo kwa kuhamasisha wananchi wa Simiyu kutumia rasilimali ardhi na mifugo ili kujikwamua kutoka kwenye umaskini, uduni wa elimu, utegemezi na unyanyasaji utokanao na kukosa kipato.
Kwa upande mwingine Taasisi inatoa elimu ya kujitambua itakayo saidia wananchi kupata viongozi bora watakao shirikiana nao katika kuleta maendeleo ya kweli ya kiuchumi, kijamii, kijinsia na kiutamaduni ikizingatiwa kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa viongozi wetu wa taifa.
Taasisi pia inatambulisha kozi zake mbalimbali inazotoa kwa wanasimiyu na kuelezea namna zilivyo na umuhimu kwa jamii kulingana na matatizo yanayojitokeza katika jamii zetu za kitanzania. Maelezo ya sifa za kujiungana na kozi hizo pia yanatolewa pamoja na udahili unafanyika hapohapo katika dawati la Taasisi katika viwanja vya nane nane Simiyu.
Kozi zinazotolewa na Taasisi ni kozi za Ustawi wa Jamii, Mahusiano kazini na Menejimenti ya Uma, kozi ya Menejimenti ya Rasilimali watu, na kozi ya usimamizi wa biashara, kuanzia ngazi ya astashahada mpaka shahada ya kwanza na ngazi ya shahada ya uzamili kwa kozi Ustawi wa Jamii na Menejimenti ya rasilimali watu ya kimkakati. Wateja wanaofika katika dawati la Taasisi wanaelezwa umuhimu wa taaluma hizi katika kuondoa umaskini na kuboresha maisha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...