Charles James, Michuzi TV

KATIKA kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia, Ofisi ya Rais-Tamisemi imeanzisha Kituo cha huduma kwa wateja ambapo sasa watakua wakihudumia wananchi kidigitali.

Mfumo huo mpya wa utoaji huduma utawasaidia wananchi kutotembea umbali mrefu kuzifuata ofisi za Tamisemi na badala yake sasa watakua wakipiga simu, kutuma barua pepe, ujumbe mfupi na kutumia mitandao ya kijamii katika kupata huduma.

Akizungumza wakati wa kuzindua huduma hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo amesema mabadiliko hayo ya kimfumo yanaifanya wizara hiyo kuendelea kuwa mfano kwa utendaji kazi wake huku akiongeza kuwa malengo yao ni kuwa na Televisheni ya Tamisemi.

" Ndugu Katibu Mkuu Mhandisi Nyamhanga nikupongeze kwa kuisogeza Tamisemi kiganjani kwa wananchi wetu, lakini sasa ili wazidi kujua kazi kubwa inayofanywa na Ofisi ya Rais-Tamisemi lazima tuwaletee TV ambayo itakua ikirusha vipindi vyetu," Amesema Jafo.

Waziri Jafo amesema kupitia kituo hicho sasa wananchi waliopo mbali hawatopata tabu tena ya kusafiri umbali mrefu wakitumia nauli kufuata huduma badala yake sasa watapiga simu na kuhudumia bila mashaka yoyote huku akiwataka watumishi wanaohudumia wananchi kupitia huduma hiyo kuwa na lugha nzuri kwa wateja.

" Hapana shaka wako watu walikua wanasafiri kutoka Kankoko Kigoma kuja Dodoma kufuatilia matokeo ya mtoto wake wengine wanasafiri Nachingwea kuja kufuatilia uhamisho wake, wanatembea umbali mrefu wanamaliza Nauli na bado wakifika hapa wanakutana na vishoka.

Sasa kupitia mfumo huu hata vishoka vitaondoka na wananchi wetu watahudumia vizuri na kwa haraka bila gharama zozote, ombi langu kwenu jitahidini kuwa na lugha nzuri hata kama mna mawazo yenu yawekeni pembeni mfanye kazi mkiweke maslahi ya watanzania mbele," Amesema Jafo.

Akizindua hiko Jafo amezitaja namba za Jafo akizindua kituo hicho amepata kutaja namba ya kupiga bure ili kuhudumiwa kuwa ni +255 262 160 210 huku akipokea simu ya mteja aliyepiga kuulizia matokeo ya kidato cha nne awamu ya pili.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga amemshukuru Waziri Jafo kwa kukubali kuwazinduliwa kituo hiko huku akimuahidi kwamba watawahudumia watanzania kwa ukarimu na kwa uzalendo.

Amesema kupitia mfumo huo wa huduma kwa wateja siyo tu watawaepusha watanzania kusafiri umbali mrefu bali pia watawaepusha na matapeli ambao hujifanya watumishi wa wizara.

Akitoa maelezo ya mfumo huo Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Wateja, Antelma Mtemahanji amesema kupitia mfumo huo pia unaweza kuona idadi ya wananchi waliohudumia pamoja na kuonesha utendaji kazi wa watumishi wa kituo hiko.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akizungumza na watumishi wa wizara hiyo wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja kilichozinduliwa leo na wizara hiyo jijini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akimhudumia mwananchi ambaye alipiga simu ambaye alitaka kujua ni lini matokeo ya kidato cha nne awamu ya pili yatatangazwa.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-Tamisemi, Selemani Jafo akiwa katika Chumba Maalum cha utoaji huduma kwa wateja kupitia simu ambapo huku watumishi wengine wakiendelea na kazi.
 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi, Mhandisi Joseph Nyamhanga (aliyesimama kulia) akielezea  mfumo huo wa huduma kwa wateja mbele ya Waziri Jafo leo wakati wa kuzindua mfumo huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...