Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Mara
FAMILIA ya Muasisi wa Taifa la Tanzania Mwalimu Julius Nyerere, ikongozwa na Mama Maria Nyerere imewaomba Watanzania katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu wamchague mgobea urais kwa tiketi ya Chama Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli.
Mama Maria amemuombea kura Dk.Magufuli leo Septemba 5,2020 wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea huyo wa urais zilizofanyika Mkenda uliopo Musoma Mjini mkoani Mara.
"Mheshimiwa wetu, kipenzi cha watanzania, sikuja kwa ajili ya kuzungumza , ila wamesema niongee kidogo,nimeambiwa niombe kura na mimi kura yangu ni moja, hivyo tuunganishe kura za wananchi wote ili Dk.Magufuli akaendelee kufanya kazi ya kutekeleza na kumalizia mipango waliyopanga kuifanya,"amesema Mama Maria.
Wakati mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM ukiendelea, Mama Maria Nyerere alikuwa akiufuatilia mkutano huo akiwa nyumbani kwake lakini aliamua kuomba aje kushiriki mkutano huo na hivyo alifika hapo akiwa ameongozana na watoto wake Madaraka Nyerere na Makongoro Nyerere.
Awali Madaraka Nyerere alipokuwa akizungumza mkutanoni hapo kwa niaba ya familia hiyo amesema Nyerere alikua mtu wa kwanza kukiri hajamaliza kazi ya kuleta maendeleo, yeye na Mzee Hayati Abeid Aman Karume walifanikiwa kuleta uhuru na kazi iliyokuwa imebakia ni kuleta uhuru wa kiuchumi.
"Rais Magufuli amefanya mambo mambo makubwa katika uchumi, na ingekuwa mkutano huu unarushwa live hadi Mwalimu Nyerere huko alikokuwa angeona angefurahi sana.Tumchague Rais Magufuli na namkumbusha Mama Maria akumbuke kumchagua Dk.Magufuli itakapofika Oktoba 28 mwaka huu ambayo ndio siku ya kupiga kura,"amesema Madaraka.
Kwa upande wake Makongoro Nyerere "Leo nina jambo moja, nimekuja kuomba kura , na kura haiombwi kwa muda mrefu, naomba kura zote ziwe kwa Magufuli,"amesema Makongoro na kuongeza.
"Tangu kampeni zimeanza Rais Magufuli amehimiza kufanyika kwa kampeni za kistaaruba na tangu ameanza kampeni zake kule Bahi hadi leo hii hapa Mara amekuwa anafanya kampeni za kistaarabu.Ni muungwana kweli Rais wetu,"amesema Makongoro.
Pamoja na mambo mengine Makongoro amesema amepeleka kijembe kwa vyama vya upinzani baada ya kudai waliopewa nafasi za utumishi na Rais Magufuli amewatoa jalalani."Eti aliowaaijri kawatoa jalalani , wengi wako kwenye utumishi wa umma na katika siasa, walioko Serikali amewasimamia vizuri, tumuongeze miaka mingine mitano ili kazi hiyo aiongoze vizuri.
"Asilimia 99 ya wana CCM ni wazuri, asilimia moja ndio wana mauzauza, hata kwa wapinzani nako wako vizuri, tunaye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghirwa ambaye alikuwa upinzani na aligombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
"Pia aliyekuwa Katibu Mkuu Chadema Dk.Wilbroad Slaa ambaye kwa sasa ni Balozi wetu ambaye anafanya kazi nzuri ya kutuwakilisha.Hivi hawa wametolewa jalalani,"amesema.

Makongoro Nyerere

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...