Charles James, Michuzi TV
KUFUATIA Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Benard Membe kutoa sababu za kusafiri nje ya nchi wakati kampeni zikiendelea, Mbunge Mteule wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Mariam Ditopile amemvaa akisema hafai kuongoza Nchi.
Membe leo amekiri kuwa alisafiri kwenda Dubai kwa mambo ya kikazi lakini pia akitumia muda huo kucheki afya ya mwili wake ambapo amesema amekutwa yuko imara na hana shida yoyote.
Akizungumza jijini Dodoma leo, Ditopile amesema kitendo cha Membe kwenda kucheki afya yake Dubai kimeonesha jinsi gani anavyodharau Hospitali zilizopo nchini na kwamba akiwa Rais atatumia kodi za watanzania wanyonge kwenda Ulaya kutibiwa ilihali zipo hospitali na madaktari wenye uwezo nchini.
" Amejionesha dhahiri yeye ni kiongozi ambaye hata akiumwa mafua ataenda kutibiwa nje ya nchi kwa fedha za walipo kodi maskini, aina hii ya viongozi siyo wa kuwapa Nchi maana wataenda kutumia rasimali zetu kwa maslahi yetu wenyewe.
Watanzania kwa miaka mitano wamekua mashuhuda wa jinsi ambavyo Rais Magufuli ameboresha sekta ya Afya na yeye mwenyewe hajawahi kufunga safari kwenda nje ya Nchi kutibiwa, lakini huyu mgombea wa ACT yeye anasafiri hadi Dubai kwenda kupima afya tu, Oktoba 28 twendeni tukawakatae hawa walaghai kwa kumpa Magufuli kura za kishindo, " Amesem Ditopile.
Amesema kwa miaka mitano serikali ya Rais Magufuli imeokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizokua zinatumika kutibia viongozi nje ya Nchi na matokeo yake amejenga vituo vingi vya afya, hospitali za Wilaya na kuboresha Hospitali zote kubwa ili ziweze kutoa huduma bora zenye kukidhi mahitaji ya watanzania wote.
Mbunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa wa Dodoma kupitia CCM, Mariam Ditopile akizungumza katika moja ya mikutano ya Kampeni ya Chama chake inayoendelea maeneo mbalimbali nchini.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...