MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akizungumza na
wananchi wa Kijiji cha Duga Maforoni wilayani Mkinga wakati wa uzinduzi
wa kampeni zake
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula kulia akipokeakitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa waTanga Henry Shekifu wakati alipozindua kampeni za Ubunge Jimbohilo eneo la Duga Maforoni wilayani Mkinga
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula kulia akipokeakitabu cha ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa waTanga Henry Shekifu wakati alipozindua kampeni za Ubunge Jimbohilo eneo la Duga Maforoni wilayani Mkinga
Mwenyekitiwa CCM Mkoa wa Tanga Henry Shekifu akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Kampeni za Ubunge Jimbo la Mkinga kulia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo
Dastan Kitandula
MGOMBEAUbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula akiwa ameshika ilani
ya CCM mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga
Henry Shekifu wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Jimbo hilo
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Tanga Dkt Aisha Kigoda akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hizo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Husna Sekiboko akizungumza wakati wa uzinduzi huo
MGOMBEA Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mwantumu Zodo akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi huo
MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa (MNEC) kupitia kundi la UWT Taifa Catherine Kitandula akizungumza wakati wa uzinduzi huo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
SEHEMU ya wana CCM na wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Meja Kunta akitumbuiza wakati wa kampeni hizo
MGOMBEAUbunge wa Jimbo la Mkinga mkoani Tanga (CCM) Dastan Kitandula amezindua rasmikampeni zake huku akiwaomba wananchi kumchagua tena kuwatumikia kwa kipindi chamiaka mitano ili aweze kumalizia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Kerokubwa ambazo zimekuwa zikilikabili Jimbo hilo ni suala la Maji na barabaraambapo alihaidi kuzipatia ufumbuzi wa kina wakati atakapopewa ridhaa yakuwatumikia wananchi hao
Uzinduziwa Kampeni hizo ulifanyia kwenye Kijiji cha Duga Maforoni
wilayani humo ambapo ilizinduliwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga HenryShekifu.Alisemawakati akipata ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000 Jimbo hilo lilikuwa nyumakimaendeleo lakini hadi sasa asilimia 90 ya vijiji vimeunganishiwa umeme wa Reana miradi ya maji, barabara na elimu imetekelezwa kwa asilimia kubwa.
Alisemahivi sasa baadhi ya vijiji ambavyo vilikuwa vikikabiliwa na uhaba wa majiwananchi wanapata maji safi na salama na kutolea mfano wa kijiji cha Mapatano.
Mgombeahuyo alisema Kijiji cha Doda wakazi wake wame unganishiwa maji kupitia mradi wa mabwawa uliogharimu sh 1.4.bilioni wakati kata ya Duga Sigaya wananchi wanapatamaji kutokana na mradi wa sh 1.2 bilioni.
Kitandulaambaye anatetea kiti hicho alisema iwapo atachaguliwa tena kushika ubunge wajimbo hilo atahakikisha anatia msukumo Serikaliniili mradi mkubwa wa kutoa maji Mabayani Jijini Tanga na kuyafikisha hadi mpaka wa Tanzania na Kenya wa Horohoro unatekelezwa.
Akizungumzia suala la umeme, Kitandula alisema wilaya ya Mkinga ina jumla ya vijiji 85ambapo 65 vimesha unganishiwa nishati hiyo huku vijiji 20 vilivyobaki vikiwavipo katika hatua za mwisho za mchakato wa kupatiwa umeme kupitia REA.
“Mkinichagua kushika nafasi hii nitahakikisha umeme sasa unapelekwa ngazi ya vitongojivilivyopo katika vijiji vyote 85 na mtandao wa barabara utaongezekazaidi”alisema Kitandula.
Kitandula amepewa dhamana ya kupeperusha bendera ya CCM kuwaniaubunge wa jimbo la Mkingaambapo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba 28 atapambana na Nuru Bafadhilwa CUF na Rehema Ali Mohamed wa ACT-Wazalendo.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...