Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kagera

RAIS Dk.John Magufuli ametoa maagizo kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) kuhakikisha zinafanya ukaguzi wa masuala ya usalama na sheria ili kuepuka maafa ya wanayoweza kutokea shuleni na kusababisha maafa kwa wanafunzi.

Ametoa maagizo hayo leo Septemba 16, 2020 wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kagera wakati wa mkutano wake wa kampeni za kuomba ridhaa ya kuchaguliwa tena kuwa Rais kwa kipindi cha miaka mitano mingine.

Hata hivyo kauli ya Rais Magufuli inakuja siku chache tu baada ya kutokea ajali ya moto katika Shule ya Msingi ya Wavulana Biamungu Islamic iliyopo mkoani Kagera ambapo wanafunzi 10 wamepoteza maisha kwa kuteketea kwa moto na wengine sita walijeruhiwa.

"Natoa maagizo kwa mamlaka mbili za Wizara ya Elimu na TAMISEMI kuanzia sasa shule zote nchini ziwe zinazingatia matakwa ya kiusalama na kisheria kabla na baada ya shule kuwa na wanafunzi, na haya maagizo yaanze kutekelezwa haraka , tunataka wanafunzi wetu huko mashuleni wawe salama,hizi ajali za shule kuungua moto zisitokee tena"amesema Rais Magufuli ambaye pia ni Mgombea urais kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu wa 2020.

Wakati huo huo Dk.Magufuli ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kumuachia Mkuu wa Shule hiyo ambaye wanamshikilia tangu ilipotokea ajali ya shule hiyo kuungua kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi hao ambapo ameshauri akaachiwe wakati wakiendelea na uchunguzi wao.

"Nafahamu Mkuu wa Shule ameshikiliwa na Jeshi la Polisi, Mkoa wa Kagera, naomba wamuachie wakati wanafanya uchunguzi, kwani hata akiwa nje bado ataendelea kutoa taarifa na ushirikiano ili kufanikisha uchunguzi wa tukio hilo,"amesema Rais Magufuli.

Amefafanua Mkuu wa Shule hiyo hana nia mbaya kiasi cha kuamua kuchoma watoto ambao amekuwa akiwalea kama watoto wake pamoja na kuwasomesha."Yeye alianzisha shule kwa ajili ya kusomesha watoto, kumuweka mahabusu ni kumuongezea machungu wakati alikuwa akiwalea vizuri kama watoto kama wake."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...