Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Chato
KAMPENI
za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)zimeingia mzunguko wa pili
kwa kishindo baada ya mgombea wake Dk.John Magufuli kufanya mkutano
katika wilaya ya Chato mkoani Geita na kuhudhuria na maelfu ya wananchi.
Katika
mkutano wa kampeni uliofanyika leo Septemba 14,2020 katika viwanja vya
Mazaina wilayani hapa, Dk.Magufuli ametumia nafasi hiyo kuelezea mipango
na mikakati ambayo yeye na Chama chake wanakwenda kuitekeleza iwapo
watapata ridhaa ya kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano ijayo baada ya
kufanya kazi kubwa ya maendeleo kwa miaka mitano iliyopita.
Dk.Magufuli
alikuwa katika mapumziko ya siku tano wilayani hump tangu Septemba 9
mpaka leo Septemba 14 mwaka huu.Akizungumza zaidi kuhusu kampeni
Dk.Magufuli amesema baada ya kufanya kazi ya kuleta maendeleo kwa
mafanikio makubwa kwa kushirikiana na Watanzania wote sasa anarudi tena
kuomba ridhaa kwa mara nyingine tena ili aendelee kuwatumikia na kuleta
maendeleo zaidi .
"Hapa
Chato watoto wengi walikuwa hawaendi shule, wakati nasoma tulioenda
sekondari tulikuwa wawili, sio kwamba wale waliokosa nafasi ya kwenda
sekondari hawakuwa na akili, walikuwa nazo lakini shule zilikuwa
hazitoshi. Tukaamua kutafuta fedha ili watoto wasome , tukabana mafisadi
na watoto wanasoma bure
"Katika
kipindi cha miaka mitano Sh.trilioni 1.09 kwa ajili ya kutoa elimu
bure, lakini Sh.bilioni 450 kwa ajili ya wanafunzi wa Vyuo Vikuu, lengo
ni kuhakikisha Taifa hili linakuwa na watu waliosoma,"amesema
Dk.Magufuli
amesema kutokana na maendeleo waliyoyafanya wilaya ya chato imeweza
kuwa na maendeleo zaidi hata ukiangalia shule ya chato kwa sasa hadi
imezungushiwa ukuta.
Ameeleza
namna ambavyo Serikali imefanha mambo makubwa katika sekta mbalimbali
ikiwemo miundombinu ya barabara,maji, afya, usafiri wa anga,usafiri wa
anga,usafiri wa majini katika maziwa makuu, ujenzi wa madara makubwa na
madogo."Ndio maana tunakuja tena kuomba ridhaa mtupe tena miaka mitano."
Akimzungumzia
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chato,Dkt.Melard Kalemani amesema alimwambia
huenda usionekane jimboni kutokana na majukumu aliyompa ya kusimamia
Wizara ya Nishati nchini na amefanya kazi nzuri na amekuwa akifanya kazi
nchi zima.
Amesema
alishangaa walipoona watu 60 kuchukua fomu za kugombea Ubunge."
Tunahitaji watu wanaofanya kazi na wala hatuchagui sura hivyo wanachato
mchagueni kalemani kwa kura nyingi ili akasimamie miradi ambayo
anayoijua.
"Msidanganywe na watu wanaokaa vijiweni,mnataka akawe anasafisha viatu na kunywa kahawa,"amehoji.Aidha amemuagiza Dkt.Kalemani kupeleka mataa ya Barabarani katika jimbo la Bukombe.
Amesema
mafanikio yote yanayofanywa na serikali ni kutengeneza maisha ya baadae
ya watoto, kwani inawezekana kwa umri wao wasifaidi hayo,ila kwa miaka
ijayo ikawa inamanufaa kwa watoto wa vizazi vijavyo.
Mgombea
wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wananchi wakati akiondoka katika viwanja vya Mazaina mara baada ya
kuwahutubia wananchi wa Chato mkoani Geita.
Mgombea
wa Urais kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia
wananchi wa Chato





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...