NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba
amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawana sababu ya kutokipigia Kura chama Cha
mapinduzi CCM kutokana Kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho kwa kipindi Cha
miaka mitano.
Naibu waziri wa Kilimo Mgumba
amebainisha hayo wakati akizungumza katika kikao Cha Halmshauri Kuu Maalum ya
Wilaya ya Morogoro Vijijini,iliyokutana kwaajili ya kuwaleta wanachama wa CCM
pamoja ili kuhakikisha chama hicho kinaibuka na ushindi wa kishindo kuanzia udiwani
Ubunge na Urais.
Mgumba ambae aligombea kuteuliwa
kuwa mbunge la Morogoro Kusini Mashariki na kupata Kura 242, ambapo Hamis
Taletale (Babu Tale ) alibuka mshindi na kuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo Hilo na
kwa sasa ni mbunge mteule kutokana na
kupita bila kupingwa katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki
Omary Mgumba amesema Sasa ni wakati
wa kuondosha makundi ya kisiasa kwa kuhakikisha chama Cha Mapinduzi CCM
kinapata Ushindi wa kutosha
Mgumba pia amesema Innocent
Kalogelesi Mbunge Mteule wa Morogoro Kusini na Hamis Taletale wa Morogoro Kusini Mashariki
wananafasi kubwa ya kuhakisha hakuna makundi kwa kuwawake watu kuwa pamoja Mara
baada ya kumaliza kwa michakato ya kumpata atakae peperusha bendera katika
majimbo ya Morogoro Kusini,na Kusini Mashariki.
Katika hatua nyingine amesema kuwa
watahakikisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dakta John Magufuli anapata kura za
kutosha kutoka majimbo hayo.
Amesema kuwa wanaimaani kubwa kuwa
majimbo hayo yataongoza kwa kumpigia kura Magufuli kutokana na kile ambacho
amekifanya ndani ya Miaka mitano
Sanjari na hilo ameongeza kuwa ilani
ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 imegusa sekta zote muhimu zenye kuja kumkoambo
mwananchi.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...