Na Karama Kenyunko, Michuzi TV

MSHTAKIWA Khamis Luwoga (38) maarufu kwa jina la Meshack anayedaiwa kumuua mke wake na kisha kuuchoma mwili wake kwa magunia mawili ya Mkaa hadi kuwa majivu amejikuta akipata na kigugumizi baada ya kukumbushiwa shtaka lake hilo na kuulizwa kama ni kweli ama si kweli alifanya mauaji hayo.

Mahakama Kuu iliyoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi, leo Oktoba 21,  ilimkukumbushia mshtakiwa shtaka lake wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali ambapo inadaiwa  Mei 15, 2019 khamisi alimuu mke wake Naomi Marijani,  

Mshtakiwa alipoulizwa kama ni kweli ama si kweli, alipata kigugumizi na kukaa  kimya
Mahojiano yake na Hakimu Shahidi yalikuwa:

Hakimu: mshtakiwa umesikia shtaka linalokukabili je ni kweli ama si kweli
Mshtakiwa: kimyaaa... nipe nafasi niweze kuelezea machache.

Hakimu: Ni kweli ama si kweli?
Mshtakiwa alikaa kimya kisha akasema... kwa bahati mbaya ni kweli kilitokea kifo cha mke wangu
Hakimu: hapa wanasema ulimuua mke wako unatakiwa kujibu kama ni kweli ama si kweli
Mshtakiwa: ni kweli alikufa kutokana a ugomvi kati yetu.
Hakimu: ni kweli mkeo alikufa unaambiwa ulimuua kwa kukusudia
Mshtakiwa: hapana sijamuua kwa kukusudia.
Kufuatia majibu hayo mahakama iliona mshtakiwa amekana makosa yake na ndipo maelezo ya awali yakasomwa

Akisoma maelezo hayo, wakili Ashura Mzava amesema, mshtakiwa
Khamis na Naomi walikuwa ni mke na mume waliobarikiwa kuwa na mtoto mmoja wa kike.

Imedaiwa kuwa, mshtakiwa alikuwa na historia  ya kumpigia mke wake mara kwa mara na huku mara nyingine akitishia kumuua.

Mei 15, 2019 huko Gezaulole Kigamboni jijini Dar es Salaam, majira ya saa moja asubuhi mshtakiwa alimpiga mke wake Naomi hadi kupelekea mauti.

Imedaiwa, baada ya kumuua mke wake, mshtakiwa alikuwa akijifungia ndani ya nyumba yake huku akifanya mbinu mbali mbali za kuweza kuharibu ushahidi hivyo
alinunua magunia mawili ya Mkaa pamoja na lita tano za mafuta ya taa huku akizuia mtu yoyote kuingia eneo la nyumba yao .

Imeendelea kudaiwa kuwa, baada ya mauaji hayo mshtakiwa alichimba shimo ndani ya eneo la nyumba yao na kuburuza mwili wa marehemu mpaka ndani ya shimo hilo na kisha kuuchoma moto mwili huo hadi kuwa majivu na baada ya hapo, alitumia gari lake aina ya Subaru forester T 206 CEJ na kuchukua majivu ya mwili ule pamoja na mabaki mengine ya mwili wa marehemu na kwenda kuyazika Mkuranga shambani kwake kwa usiri wa hali ya juu.  

Amedai kuwa, tukio hilo liliripotiwa Central polisi na baada ya uchunguzi wa kina kufanyika, mshtakiwa alikamatwa  ambapo baada ya upekuzi  kufanyika nyumbani kwa mshtakiwa na shambani kwake kulipatikana matone ya damu, baadhi ya vipande vya mwili wa mwanadamu pamoja na majivu.

Vitu vyote hivyo, vilifungwa kwa pamoja na kupelekwa kwenye maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kumpima DNA  ambapo majibu alipotoka yaliendana na vinasaba vya ndugu wa marehemu.

Katika mahojiano yake na polisi, mshtakiwa alikiri kumuua mke wake na ili kuficha ushahidi aliuchoma moto mwili wake nyumbani kwake kwa kutumia mkaa


Hata hivyo upande wa mashtaka umesema jumla ya mashahidi 28 wanatarajiwa kufika mahakamani hapo kutoa ushahidi na pia watakuwa na vielelezo  sita.

Kesi hiyo itaanza kusikilizwa baada ya kupangiwa tarehe  nyingine.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...