Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

BODI ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) wametoa pongezi kwa Mamlaka hiyo kwa kuweza kutunza chanzo cha maji cha Mto Kizinga chenye zaidi ya miaka 70.

Chanzo hicho kilichoanzishwa maaka 1950, kimeweza kuendelea kutoa huduma ya maji kwa baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar Es Salaam.

Katika ziara hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ikiongozwa na Mwenyekiti  wake, Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange wameweza kupata taarifa mbalimbali za Mtambo huo kuanzia kwenye chanzo hadi uzalishaji.

Akitoa ufafanuzi wa Bodi ya wakurugenzi, Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Dawasa Mhandisi Shaban Mkwanywe

amesema mtambo wa Kizinga ulianza na uzalishaji maji  lita 7000 na ulikua na changamoto ya kukauka maji na kupelekea kuzimwa mtambo mara kwa mara.

Amesema, wamefanyia marekebisho mtambo huo ikiwemo na kulinda chanzo cha maji na kupelekea kutokuzimwa kwa mtambo huo mara kwa mara na uzalishaji kufanyika kwa muda wote.

Mkwanywe amesema, kwa sasa mtambo wa Mtoni unazalishaji maji lita Milioni 9 kwa siku na unahudumia baadhi ya maeneo ya Dar Es Salaam ikiwemo Chang'ombe, Mtoni, Mtoni Kijichi hadi Kurasini.

"Mtambo huu ni wa zamani na ndio ulikua chanzo kikuu cha maji kwa Mkoa wa Dar Es Salaam, ulianza kwa Lita 7000 kwa siku ila sasa tunazalisha maji Lita milioni 9 kwa siku," amesema.

Baada ya taarifa fupi, Bodi ya Wakurugenzi walitembelea chanzo cha Mto Kizinga hadi uzalishaji wa maji na kupata maelezo kutoka kwa wataalamu wa Dawasa.

Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange  wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Dawasa Mhandisi Shaban Mkwanywe (wanne kulia) walipotembelea Mtambo wa Uzalishaji maji na Chanzo cha Mto Kizinga, Mtoni Mashine ya Maji Jijini Dar Es Salaam.


Mtaalamu wa Masuala ya Maabara Dawasa, Ali Mpili akitoa maelezo kwa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake  Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange walipotembelea Mtambo wa Uzalishaji maji na Chanzo cha  Mto Kizinga, Mtoni Mashine Mashine ya Maji Jijini Dar Es Salaam

Bodi ya Wakurugenzi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange  wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Dawasa Mhandisi Shaban Mkwanywe (wapili kushoto) walipotembelea Mtambo wa Uzalishaji maji na Chanzo cha Mto Kizinga, Mtoni Mashine ya Maji Jijini Dar Es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...