Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
BONDIA wa Tanzania Twaha Kassim Rubaha ' Kiduku' anatarajia kushuka ulingoni Oktoba 30 kupambana na Bondia Sirimongkhon Lamthuan kutoka Thailand.
Akitambulisha pambano hilo, Mkurugenzi wa Golden Boy Africa Shomar Kimbau amesema Twaha Kiduku atashuka ulingoni kugombani mkanda wa WBC (World Boxing Council) dhidi ya Bondia kutoka Thailand.
Amesema, pambano hilo litakuwa na mapambano sita ya utangulizi kabla ya kuanza kwa pambano hilo la ubingwa wa WBC.
"Oktoba 30, Twaha Kiduku atashuka ulingoni kupambana na Bondia Lamthuan kutoka Thailand na atawasili nchini Oktoba 24," amesema.
Kimbau amesema, baada ya bondia huyo kuwasili, Oktoba 25 watakutanishwa na Oktoba 29 watapima uzito kabla ya kupanda ulingoni.
Aidha, kwa upande wa Bondia Twaha Kiduku amesema amejiandaa vizuri katika pambano hilo na anaendelea na ratiba ya mazoezi kama kawaida.
Kiduku amesema, anafahamu mpinzani wake ni mzuri ameweza kucheza mapambano 101, mapambano 97 akiwa ameshinda na manne kupoteza.
"Nafahamu mpinzani wangu ni bora mapambano zaidi ya 60 ameshinda kwa KO kati ya 97 na akipoteza minne tu," amesema
Kiduku ameeleza kuwa atashuka ulingoni kuhakikisha ubingwa wa WBC unabaki nyumbani.
Pambano hilo linatarajia kufanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba, na litakuwa na pambano la utangulizi kutoka kwa Alphonce Mchumia Tumbo vs Jongo Jongo, Maono Ally vs Joseph Sinkala.
Mapambano mengine ni Said Juma vs Ibrahim Tamba, Said Wigo vs Francis Miyeyusho, Hamza Iddy Shaban vs Jamal Kunoga na Ruth Chisale vs Sijali Said.
Bondia Twaha Kiduku akizungumzia pambano la kugombania mkanda wa WBC (World Boxing Council) dhidi ya Bondia Sirimongkhon Lamthuan kutoka Thailand litakalofanyika Oktoba 30 kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...