Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA.)
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
JAJI Mkuu wa Mahakama ya
Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma ametoa pongezi nyingi kwa Baraza
la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kwa usimamizi wake madhubuti
katika kutoa mafunzo mbalimbali ya kujengea uwezo wa kiweledi na kiutendaji kwa
watumishi wa Mahakama Tanzania.
Jaji Mkuu ametoa
kauli hiyo wakati akizindua baraza la 7
na semina elekezi kwa wajumbe wa Baraza
la Uongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto iliyofanyika Oktoba 7, 2020 Jijini
Dar es Salaam.
Jaji Mkuu amesema kwamba, Chuo cha IJA chini ya Baraza la Uongozi kimeonyesha mfano mzuri kwa kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake hasa katika kusimamia na kutekeleza malengo, huku mafunzo mengi na bora yakifanyika chini ya usimamizi wa Chuo sehemu mbalimbali za Nchi.
Amesema kuwa, kati ya mafunzo hayo ni yale ambayo yalifanyika kwa ajili ya kuwajengea
uwezo Maafisa wa Mahakama ili kuweza
kukabiliana na mashauri ya uchaguzi, hiyo imekuja na sambamba kabisa na kipindi
hiki ambacho Nchi yetu inaingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa viongozi.
Aidha, aliongeza kuwa Chuo
kimeendesha mafunzo mbalimbali. Kati ya mafunzo hayo ni pamoja namna bora ya uendeshaji wa
mashauri ya mtoto ambayo yalitolewa kwa zaidi ya wadau 1000 nchini, Kutokana na Sera ya Mafunzo ya mwaka 2019
Mahakama ya Tanzania imetoa Jukumu kwa IJA kuratibu Mafunzo yote endelevu kwa
Watumishi wa Mahakama.
“Huu ni wakati wa IJA kujiimarisha ili Chuo kitoe Mafunzo kwa watumishi wa mahakama katika eneo la utoaji haki mtandao” amesema hayo Jaji Mkuu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...