Mkurugenzi wa Shule zinazoongozwa na Mutembei Holding Limited (HML), Peter Mutembei akizungumza katika mahafali ya 20 ya kidato cha nne katika Shule ya Sekondari St. Matthew's yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Wilani Mkuranga.
Mgeni Rasmi, Afisa Elimu Mkoa wa Pwani, Hadija Mcheka akitoa zawadi kwa baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri kwenye baadhi ya masomo katika Shule ya Sekondari St. Matthew's katika mahafali ya 20 ya shule hiyo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 3, 2020 Wilayani Mkuranga.
Na Avila Kakingo, Michuzi TV
IMEELEZWA kuwa wazazi waliopeleka watoto wao katika shule ya St. Matthew's watajivunia matunda bora kutoka kwa wanafunzi wanaohitimu elimu ya Sekondari katika shule hiyo iliyopo iliyopo Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.
Akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari St. Matthew's, yaliyofanyika Mwishoni Mwa wiki Oktoba 3, 2020 Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Peter Mutembei alisema kuwa wanafunzi wa shule hiyo wameweza kutengeneza Kiyoyozi kinachotoa manukato pamoja Bajaj inayotumia upepo wakati wa ufanyaji kazi wake sambamba na wanafunzi kujifunza kupiga picha.
Mutembei amesema kuwa hayo yote wanafunzi wamewezeshwa na kushirikiana na walimu waliopo katika shule hiyo.
"Naamini muda sio mrefu Wazazi mtaacha kuingia gharama za kukunua bidha za watu wengine mtaanza kutumia bidhaa za watoto wenu waliosoma katika Shule zetu. "Alisema Mutembei.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari St. Matthew's, Joseph Nalaila alisema kuwa taaluma ya Shule ya Sekondari St. Matthew's inakwenda sambamba na mafunzo ya nje ya madarasa hasa kutembelea mbuga za wanyama, kutembelea viwanda pamoja na ziara nyingine za kimasomo.
Hata hivyo alisema mwenendo wa ufaulu wa wanafunzi katika miaka mitatu mfululizo ni mzuri kwani kwa mwaka 2018 shule hiyo mtihani wa taifa wanafunzi walifaulu kwa asilimia 98.5, kwa mwaka 2019 mtihani wa taifa wanafunzi walifaulu kwa asilimia 99.1 na kwa mtihani wa kujipima kwa 2020 Mtihani wa Mock wanafunzi walifaulu kwa asilimia 100 kwani wanafunzi wote walifaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu.
hata hivyo Mwalimu Nalaila alisema kuwa, Shule hiyo ina kufudisha lugha ya Kichina kwa wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita.
Alisema kuwa kwa wanafunzi 10 waliosoma Shule ya Sekondari St. Matthew's na kufanya vizuri wanasoma nchini China kwa ngazi mbalimbali za masomo kwa ufadhili wa serikali ya China.
Licha ya hayo Shule ya Sekondari St. Matthew's, kwa mwaka wa masomo 2020 wahitimu 136 wa kidato cha nne wakiwemo wasichana 66 na wavulana 66 inakwenda sambamba na kauli mbiu ya kuwa na elimu bora, Malezi Bora, Haki na Usalama kwa Mtoto pamoja na mafunzo ya ziada, ziara za kimasomo na michezo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...