Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imemaliza maandalizi yake ya mchezo wa mzunguko wa sita dhidi ya Timu ya Cost Union ya Tanga mchezo utakaopigwa katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

Kaimu Kocha wa Timu hiyo,Habibu Kondo amesema kuwa kikosi hicho kwasasa kimefanya maandalizi ya kutosha kwa asilimia kubwa na hivyo kiko tayari kwa mchezo huo wa kesho.

Kocha Habibu amesema anauhakika na maandalizi ambayo ameyafanya katika kipindi ambacho ligi ilisimama kwa muda na kwamba anakiamini kikosi hicho kuwa kitaleta matokeo mazuri katika mchezo wa kesho.

Ameongeza kuwa katika mazoezi hayo, ametumia nafasi hiyo kurekebisha makosa madogo madogo ambayo yalijitokeza katika michezo mwili na hivyo kupelekea kupoteza na kwamba mechi ya kesho itakuwa na ushindi mkubwa.

" Kikosi kimefanya mazoezi ya kutosha tunaimani kuwa katika mchezo wa kesho tunakwenda kupata matokeo mazuri kama ilivyo kawaida ya KMC FC, kwasababu uwezo wakushinda mechi hiyo tunao kwa asilimia 100" amesema Kocha Habibu.

Katika hatua nyingine Mchezaji wa KMC FC ambaye alikuwa majeruhi kwa muda mrefu, Sadala Lipandike ameanza kufanya mazoezi mepesi na Timu Leo kutokana na Afya yake kukaa vizuri.

Sadala alikuwa anasumbuliwa na goti na kwamba hivi sasa ameanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo mingine ya Ligi kuu soka Tanzania Bara.









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...