Alisema hiyo ni mara nyingine tena kwa kampuni yao wakishirikiana na Lions Club kusaidia jamii yenye uhitaji. Tulifanya hivi kwenye hospitali ya wazee Kinyerezi, pia wakati wa maadhimisho ya ugonjwa wa kanda duniani, tulitembelea na kuwafariji wagonjwa katika Taasisi ya Kansa ya Ocean Road Dar es Salaam.

KAMPUNI ya kubashiri matokeo ya Meridian Bet na klabu ya Lions, zimesaidia kampeni ya upimaji,matibabu na ushauri nasahaa ya magonjwa ya macho, sukari na shinikizo la damu, yaliyotolewa bure jana Jumapili kwenye hospitali ya Polisi Kilwa road, Dar es Salaam.

 Kampeni hiyo iliyollenga kutoa miwani bure kwa wagonjwa ambao madaktari waliwataka kutumia baada ya vipimo, iliwahusisha mamia ya wakazi wa jijini Dar es Salaam.

 Mganga mkuu wa hospitali hiyo na mkuu wa kikosi cha afya cha polisi nchini, Dk Hussein Yahya alisema muitikio wa Watanzania waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo umekuwa mkubwa tofauti na ilivyotarajiwa.

 Hadi saa 3 Asubuhi, watu 456 walikuwa wamejiandikisha kupatiwa huduma hiyo wakiwamo watoto na wazee, huku Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi, Kihenya Kihenya akiwaomba wadhamini wao, kampuni ya Meridian Bet na klabu ya Lions, kampeni hiyo kuwa endelevu.

"Meridian Bet na Lions club wameonyesha njia, natamani kampeni hii iwe endelevu," alisema ACP Kihenya ambaye alitunukiwa nishani ya ugavana na kuwa balozi wa Lions Club.

Alisema wadhamini wa kampeni hiyo, kampuni ya Meridian Bet na klabu ya Lions wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kujitoa kwao katika jamii.

Meneja Uendeshaji wa Meridian Bet, Carlo Njato alisema wameamua kusaidia kampeni hiyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya.

"Tumeleta dawa, vipimo vya sukari, thermometer, miwani za jua na za kuonea na vifaa tiba mbalimbali ili usaidia kampeni hii," alisema Njato.

 Alisema ushiriki wao kwenye kampeni ya matibabu ya macho katika hospitali ya Polisi Kilwa Road ni muendelezo wa kampuni kurudisha kwa jamii, lakini pia wanaunga mkono juhudi ambazo Serikali imekuwa ikifanya katika sekta ya afya nchini.

 Gavana wa klabu ya Lions Tanzania, Moiz Bakari alisema klabu yao imekuwa ikijitoa kwa jamii na hiyo ni sehemu ya majukumu wanayoyafanya. Alisema klabu yao nchini Tanzania ina wanachama 660 ambao wamekuwa wakijitoa na kusaidia jamii yenye uhitaji katika nyanja tofauti ikiwamo ya afya, elimu na masuala mengine ya kijamii.

"Tunatamani watu wengi zaidi wajitokeze na kujiunga na klabu yetu kwa ajili ya kujitolea na kufanya kazi za jamii," alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...