Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WAKALA wa Huduma za Misitu nchini (TFS) umetoa wito kwa Wananchi wa maeneo mbalimbali hususan maeneo ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaonana na Wenyeviti wa Vijiji pindi wanapotaka kuchoma moto mashamba yao kwa lengo la kuandaa mashamba hayo.
Hayo yemeelezwa na Meneja Mawasiliano wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS), Martha Chassama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Chassama amesema kuwa miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba ni kipindi ambacho wananchi wanaandaa mashamba yao hivyo basi kuna kila sababu ya kupata elimu juu ya uandaaji wa mashamba ili kuzuia uchomaji misitu kiholela na kusababisha majanga ya moto katika Hifadhi za Misitu na kuharibu uoto asili.
"Wengi hawana elimu ya majanga ya moto, sisi kama TFS kwa kushirikiana na Wenyeviti wa Vijiji tutasaidia kutoa elimu na kuhakikisha elimu hiyo inawafikia Wananchi hao pindi wanapotaka kuandaa mashamba yao."amesema Chassama.
Pia Chassama ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha pindi wanapochoma moto mashamba hayo wasikubali kuachia moto huo kutoroka kuelekea sehemu mbalimbali na kuleta madhara kwa kuharibu Hifadhi za Misitu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...