Na Mwandishi wetu, Manyara
TAASISI
ya Kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, imejipanga
kuhakikisha inafuatilia na kuzuia rushwa kwenye kipindi hiki cha kampeni
za vyama na uchaguzi mkuu.
Naibu
Mkuu wa TAKUKURU mkoani Manyara, Isdory Kyando ameyasema hayo mjini
Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya taarifa ya
utendaji kazi kuanzia mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu.
Kyando
amesema wanafuatilia na kuzuia vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi mkuu
ili kuepuka kuchagua viongozi wasiofaa kutokana na vitendo vya rushwa.
Amesema
TAKUKURU imejipanga kuendelea na majukumu yake katika robo ya Oktoba
hadi Desemba 2020 ambapo pamoja na mambo mengine kipaumbele kitakuwa
katika maeneo yafuatayo.
Amesema wataendelea na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari.
``Tutaendelea
kufuatilia kwa karibu maendeleo ya watumishi wanaolalamikiwa mara kwa
mara na tutafanya uchunguzi wa kina dhidi yao na kuchukua hatua stakii
za kisheria,`` amesema Kyando.
Amesema
katika kuelimisha umma wametoa jumla ya semina 56 zilizoendeshwa kwenye
makundi tofauti ili kuelimisha jamii katika kupambana na rushwa.
Amesema wamefanya jumla ya mikutano 56 ilifanyika ikiwa na madhumuni ya kuelezea athari za rushwa na namna ya kupambana nayo.
``Jumla
ya makala mbili ziliandikwa, makala hizi hutolewa katika jarida jarida
la TAKUKURU ambalo hutolewa kila baada ya miezi mitatu,`` amesema
Kyando.
Amesema TAKUKURU
imekuwa sehemu ya kuimarisha vyama vya ushirika, kabla TAKUKURU
haijaingilia urejeshwaji wa fedha za vyama vya ushirika vyama vingi
vilikuwa taabani kifedha kiasi cha kushindwa kutekeleza majukumu na
kufikia malengo kwa kuwa fedha nyingi zilikuwa mikononi mwa watu na
hawakuwa tayari kuzirejesha.
Amesema
kuongezeka kwa ushiriki wa wana Manyara kwenye mapambano dhidi ya
rushwa, kutoa taarifa hasa baada ya kazi kubwa kuonekana ikiendelea
kufanyika katika kusimamia haki na kudhibiti vitendo vya rushwa na
ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.
Amesema
awali taarifa zilizokuwa zinapokewa zilikuwa chache ukilinganisha na
sasa na taarifa hizi wamezipima na kubaini kuwa siyo kwamba vitendo vya
rushwa vimeongezeka bali zimetokana na mwamko na ujasiri wa wana Manyara
kutoa taarifa TAKUKURU kila wanapokutana na changamoto.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...