Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitangaza kukamilika kwa udahili wa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili, Oktoba 9, 2020.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kukamilika kwa udahili wa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili kwa mwaka wa masomo wa 2020/2021 katika mkutano uliofanyika leo Oktoba 9, 2020 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hizo jijini Dar es Salaam,  Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa uratibu wa Udahili na utunzaji wa Kanzidata wa Time hiyo Dkt. Kokuberwa Kulunzi-mollel  na wa kwanza kulia ni Mkaguzi wa Mahesabu ya ndani wa TCU Lucy Mrikaria.
Mkurugenzi wa Ithibati wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Dkt Telemu Kassile (aliyevaa suti) na Mwana Sheria wa Tume hiyo Roserine Rutta, Kushoto wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Prof. Charles Kihampa (hayumo pichani) wakati wa Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Ijumaa Oktoba 9, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Na Karama Kenyunko,  Globu ya jamii.

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufungua kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2020/2021 utakaokuwa kwa siku sita kuanzia Oktoba 12 hadi 18 mwaka huu.

Pia tume imewasisitiza waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi yao ya udahili na kudahiliwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbali mbali kutumia fursa hiyo kwa kutuma maombi yao ya udahili kwa vyuo wanavyovipenda.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof.Charles Kihampa amesema hayo leo Oktoba 9, 2020 alipokuwa akitangaza kukamilika kwa udahili wa awamu ya kwanza na kufunguliwa kwa awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza 2020/2021

Kufuatia kufunguliwa kwa awamu ya pili, tume pia imezielekeza Taasisi za Elimu ya Juu kutangaza programu ambazo bado zina nafasi huku waombaji wa vyuo pia wakihimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili. 

“Waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyotolewa na TCU kama inavyooneshwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).” Amesema Prof.Kihampa.

Aidha Prof.Kihampa amesema kuwa katika awamu ya kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 90,572 walituma maombi ya kujiunga katika vyuo 74 vilivyoidhinishwa kudahili huku programu 686 zikiwa zimeruhusiwa kudahili ukilinganisha na programu 645 mwaka 2019/2020 na kwamba mwaka huu kuna jumla ya nafasi 157,770 ikilinganishwa na nafasi 149,809 za mwaka uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7,961 za shahada ya kwanza sawa na asilimia 5.3

"Katika awamu hii ya kwanza ya udahili jumla ya  waombaji 60,621 sawa na asilimia 69.9 wamepata udahili vyuoni  hii ni inaonyesha ongezeko la wahitimu kidato cha sita na stashahada", amesema Prof. Kihampa.

Aidha Tume imewataka waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja kuthibitisha udahili wao kwa kuchagua chuo kimojawapo kuanzia leo Oktoba 9 hadi 17 2020.

Amesema waombaji hao watatumiwa ujumbe mfupi kupitia simu ama barua pepe zao walizotumia kuomba udahili  ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...