Na Mary Gwera, Mahakama
Muonekano katika picha, maendeleo ya ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki ‘IJC’s’ katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Morogoro, Mwanza, Kinondoni na Temeke.
Kwa mujibu wa Bw. Fabian Kwagilwa, Mhandisi Ujenzi-Mahakama ya Tanzania amesema kwa sasa hatua ya ujenzi iliyofikiwa katika vituo hivyo ni ya umaliziaji 'finishing' na kazi za nje 'external works' na ujenzi wa vituo hivyo unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Ujenzi wa Vituo hivi utakapokamilika, utasaidia kurahisisha na kusogeza huduma ya haki karibu zaidi na wananchi, aidha katika vituo hivi kutakuwa na huduma mbalimbali za haki zote zikiwa zinatolewa ndani ya jengo moja. Ndani ya majengo hayo kutakuwa na ofisi za Magereza, Mawakili na wadau wengineo.
Muonekano wa jengo la Kituo Jumuishi cha utoaji haki 'Integrated Justice Centre' -Arusha.Muonekano wa 'IJC' Dodoma.
Hatua iliyofikiwa ujenzi wa 'IJC' Kinondoni-Dar es Salaam
Hatua iliyofikiwa ujenzi wa 'IJC' Morogoro.
Kazi ya ujenzi ikiendelea 'IJC' Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...