Mchungaji Shepherd Bushiri anasakwa nchini Afrika Kusini kwa mashitaka ya utakatishaji wa fedha

Waziri wa usalama wa ndani ya nchi wa nchini Malawi , Richard Banda, amesaini nyaraka kwa ajili ya mchungaji tajiri na maarufu Shepherd na mke wake, Mary, vimeripoti vyambo vya habari vya Malawi.

Hii inafuatia ombi la mahakama ya nchi jirani ya Afrika Kusini ambako Bushiri na mke wake Mary wanasakwa na mashitaka ya utakasaji wa fedha na ufisadi.

Mahakama ya juu zaidi nchini Malawi iko tayari kuamua kuhusu kukamatwa kwa wawili hao baada ya kuachiliwa huru bila masharti na mahakama ya hakimu mkazi ambayo ilisema kuwa ilichukua uamuzi huo kwasababu hapakuwa na ombi rasmi la kumrejesha lililotolewa na Afrika Kusini.

Mahakama itaamua kuhusu kesi hiyo tarehe 22 Disemba, kwa mujibu wa gazeti la Daily Times newspaper. HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...