Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV 

MBUNGE wa Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam Dk.Faustine Ndugulile amekagua mradi wa maji ambao unagharimu Sh.bilioni 10.5 uliopo Kata ya Kisarawe II.

Dk.Ndugulile amekagua mradi huo leo Desemba 2,2020 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo la Kigamboni.Akiwa katika mradi huo alikuwa ameongozana na Meneja DAWASA Wilaya ya Kigamboni Tumaini Muhondwa.

Akiwa katika ziara hiyo Dk. Ndugulile amekagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita milioni 15  ambalo litatumika kusambaza maji wilayani  Kigamboni ambapo ameonesha kuridhishwa kwa utekelezaji wa mradi huo kwa hatua iliyofikia hadi sasa.

Aidha amewataka DAWASA kukamilisha kwa haraka ramani ya mfumo wa usambazaji wa maji Kigamboni (Water Distribution network Design), pia kushirikisha Ofisi ya Mbunge katika uandaaji wa ramani hiyo.

" Nitoe angalizo kwa uongozi wa DAWASA wilaya ya Kigamboni kuanisha mapema maeneo ambayo ni akiba kwa ujenzi wa mradi wa maji siku zijazo na kuwataka kukutana na watu wa mipango miji kwa lengo la kuondoa adha kwa Serikali kuja kulipa fidia  kubwa kwa wananchi,"amesema Dk.Ndugulile.

Pamoja na hayo , amewataka DAWASA kushughulikia kwa haraka malalamiko ya wananchi yanayohusu gharama za kuunganisha maji, ankra za maji  na usimamizi wa visima vilivyorithiwa toka kwa wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...