WATU watano  wakazi wa Ukonga jijini Darves salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu Uchumi kwa kulisababishia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) hasara ya Sh. Milioni sita.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na Wakili wa Serikali Mkuu, Materus Marandu, imewataja washtakiwa hao kuwa ni, Mwalimu Boniphace Singaille(48) Twalibu Kasamu(32), Mwarami Mussa(45), Vumilia Kambi na Haidary Hassan (35).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kassian Matembele, Marandu akisaidiana na Kija Luzungana,  amedai washtakiwa hao kwa pamoja na wenzao wawili ambao ni wagonjwa wanadaiwa January 2018 eneo la Kichangani Ukonga Madafu,  waliingilia miundombinu inayotumika kutoa huduma muhimu kwa kutoa  mita ya Tanesco kutoka katika kiboksi kinachohifadhia mita na kuifunga moja kwa moja.

Imeendelea kudaiwa kuwa, kati ya Januari 18 na Agosti 2020 maeneo hayo hayo, washitakiwa wote kwa makusudi waliingilia mita ya umeme wa Tanesco na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh 6,868,910.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imewataka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili, mmoja kutoka Taasisi inayotambulika kisheria atakayesaini bondi ya Sh. Milioni moja huku mdhamini mwingine akitakiwa kuwa na barua kutoka Serikali ya Mtaa inayowatambulika ikiwa imeambatanishwa na picha ndogo ya rangi( passport).

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena, Desemba 16, 2020.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...