WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema miradi yote inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini lazima isimamiwe vizuri ili kuhakikisha inakuwa na viwango vinavyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.

 

“Maelekezo ya Serikali kwenye maeneo yote muhimu ya miradi isimamiwe kwa kina na hasa thamani ya fedha na viwango vya ujenzi wa miradi yenyewe. Tumeona Sekondari ya Tunduru, majengo ya halmashauri ya wilaya ya Mbinga, barabara ya Mbinga-Mbamba Bay na uwanja wa ndege utaalamu umetumika na thamani ya fedha ipo.”

 

Ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Januari 6, 2021) alipozungumza na viongozi wa mkoa wa Ruvuma katika Uwanja wa Ndege wa Songea akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam. Uwanja huo kwa sasa unakarabatiwa ili kuimarisha huduma za usafiri wa anga mkoani Ruvuma.

 

Amesema zaidi ya shilingi bilioni 37 zimetumika kuimarisha uwanja huo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma. Ukarabati huo umehusisha njia ya kurukia ndege yenye uwezo wa kupokea abiria zaidi ya 150, jengo la abiria na maeneo ya maegesho yenye uwezo wa kuegesha ndege kubwa sita. Uwanja huo utakapokamilika utaruhusu ndege kutua usiku na mchana.

 

Waziri Mkuu amewataka viongozi hao waendelee kuwahamasisha wananchi kutumia fursa hiyo ya uwepo wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika kufanya biashara ili kukuza uchumi wao kwa kuwa wana miundombinu ya kutosha.

 

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao wahakikishe wanasimamia matumizi ya miundombinu ya miradi mbalimbali iliyokamilika ili iweze kutumika vizuri zaidi na kwa muda mrefu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...