Watakiwa kujiunga vyama vya ushirika

 Waugaji nyuki na wafanyabiashara wa mazao ya nyuki nchini wametakiwa kuimarisha na kujiunga na vyama vya msingi vya ushirika ili waweze kunufaika na huduma zitolewazo na vyama hivyo.
 
Wito huo umetolewa jana Januari 5,2021 na Kamishna Msaidizi - Ufugaji Nyuki, Hussein Msuya alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa Jukwaa la Ufugaji Nyuki  nchini – TABEDO katika ukumbi wa Chuo cha Ushirika Moshi tawi la Dodoma.
 
Msuya alisema, baada ya Serikali kufuta kampuni  zenya ukomo wa ahadi na yasiyo na mtaji ambayo hayafanyi shughuli za kukuza biashara na ukwekezaji yaliyokiwa yamesajiliwa na msajili wa Makampuni (BRELA). TABEDO ikiwemo, imelazimika kukutana na wanachama wake kwa lengo la kujadili hatma yao na kuunda kamati itakayokwenda kufanya tathimini ya vyama vya msingi vya ushirika wa wafugaji nyuki nchini. 
 
“Hivi sasa hatuelewi “status” ya vyama vya msingi hivyo kamati hii itakayokwenda kuundwa leo itafanya tathimini kuona ni nini kinaendelea, tukishaelewa sasa tutaenda kuangalia ni nini hasa kilichopelekea vyama hivi kusinzia au kufa,
 
“na kwa kushirikiana na watu wa ushirika kamati itaangalia ni mambo gani itafanya kuhakikisha vyama hivi vinasimama na kushauri namna bora ya kuunda muunganiko utakakuwa mbadala wa TABEDO na kuja na mfumo mwingine wa kuunganisha vyama vya mushirika vya  msingi” anasema Kamishna Msaidizi huyo.
 
Msuya alitoa wito kwa wananchama kutoa ushirikiano kwa kamati itakayoundwa ili kujitendea haki kwa kile alichokisema “unakata mti unapanda mti sio unaenda kulala”. 
Azima  ya kukuza viwanda haitatimia ikiwa hakutakuwa na ushirika wa wafugaji nyuki ulio imara, ushirika  wa wafugaji nyuki utawezesha kuapta nguvu ya kukuza mitaji na kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki, ambayo ni malighafi ya viwanda vya mazao ya nyuki.
 
Rudia Issa ni Mwenyekiti wa  iliyokuwa TABEDO anasema wako tayari kushirikiana na kamati itakayoundwa ili kuweza kuunda vyama vya ushirika vitakavyokwenda kutoa ufumbuzi wa mahitaji ya wafugaji nyuki nchini.
 
Alisema kila mfugaji nyuki akitambua umuhimu wa kuwa mwanachama wa ushirika, atanufaika na mafao mbalimbali ikiwamo kupatiwa mikopo kutoka katika taasisi za fedha pamoja na soko la uhakika la mazao yake.
 
Lemiona Kimeshua ni mfugaji nyuki na mwananchama wa TABEDO anasema aliacha shughuli za ufugaji nyuki na kubaki kuwa mnunuzi kutokana na kulegalega kwa vyama vya ushirika lakini kutokana na mkazo mkubwa wa Serikali kwenye sekta hiyo ameamua kufufua na kuanzisha mashamba mapya ya nyuki.
Rudia Issa ni Mwenyekiti wa  iliyokuwa TABEDO  akiwasisitizia wanachama wake umuhimu wa kujiunga na Chama vya ushirika vilivyopo na vile vitakavyoanzishwa.
Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TBEDO  Ayubu Kamwaga na  Mwenyekiti wake Rudia Issa ni wakicheka kwa Furaha baada ya kuthibitishiwa kuzaliwa uya kwa chama hicho kama chama cha ushirika baada ya kufutwa rasmi na Serikali kwa mujibu wa Sheria.
Kamishna Msaidizi - Ufugaji Nyuki, Hussein Msuya akiwaeleza Mipambo mbalimbali ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania katika kuhakikisha wananufaika na fursa mbalimbali wanazozitoa kwa vikundi na kuwataka wajiunge ili waweze kuwa na sifa wakunufaika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...