Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari ya Wavulana Songea(Songea Boys) wakimsikiliza Afisa Huduma na Elimu kwa walipa kodi wa Mamlaka ya Mapato(TRA)Mkoa wa Ruvuma Justine Katiti(hayupo pichani) wakati wa  Utoaji wa Elimu ya kodi kwa wanafunzi hao  iliyofanyika katika ofisi za Mamlaka hiyo ambapo Tra inatoa Elimu ya kodi  katika shule mbalimbali za msingi na Sekondari mkoani humo.Picha na Muhidin Amri

…………………………………………………………………………………….

Na Muhidin Amri,Songea

MAMLAKA ya mapato(TRA)mkoani Ruvuma,imeanza kutoa elimu ya walipa kodi kwa wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari katika mkoa huo yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu  masuala mbalimbali ya kodi ili wanapomaliza masomo yao wawe walipa kodi na kuwa wawakilishi wazuri  katika masuala ya kodi.

Afisa huduma na elimu kwa walipa kodi mkoa wa Ruvuma Jastine Katiti alisema,wako katika utaratibu wa kutoa elimu kwa walipa kodi hususani katika makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo kuanzisha klabu za walipa kodi(Tax club) kwa shule  zote za sekondari.

Alisema, lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na uelewa mkubwa katika masuala mbalimbali ya kodi  ili baada ya kumalia masomo yao wawe walipa kodi ,wakusanya kodi na walimu wazuri katika masuala mbalimbali yanahusu kodi za serikali.

Alisema,kila mwaka wanatoa elimu ya kodi kwa wanafunzi wa shule sita katika wilaya zote za mkoa wa Ruvuma, na utaratibu uliopo katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza wanatembelea shule tatu na wakati mwingine wanafunzi wanafika  kwenye ofisi za Tra ili kupata elimu  ya kodi kama sehemu ya masomo yao.

Alisema ni mategemeo ya Tra kuwa,wanafunzi hao pindi watapomaliza masomo yao watakuwa wawakilishi wazuri  na walipa kodi ambao watafanya shughuli zao bila kificho au kukimbia  wanapowaona maafisa wa Tra.

Baadhi ya wanafunzi waliopata elimu ya kodi kutoka shule ya Wavulana Songea wameipongea Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini kwa  kazi nzuri inayofanya ya kukusanya mapato ya Serikali ambayo yamesaidia sana nchi kupiga hatua kubwa ya maendeleo.

Emmanuel Malagwa mwanafunzi wa kidato cha sita alisema, sasa watanzania wanatembea kifua mbele kutokana na  maendeleo makubwa, kukua kwa uchumi,kupungua kwa umaskini na kuimarika kwa huduma mbalimbali za kijamii.

Alisema, mafanikio hayo yamepatikana kutokana na mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa mamlaka ya mapato kukusanya kodi na maduhuli mengine ya serikali.

Aidha, amewataka watanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa Tra katika suala zima la kulipa kodi na ukusanyaji mapato ya Serikali kwani  matunda yake yameanza kuonekana katika maeneo mbalimbali ya nchini na kuhaidi  kuanzia sasa na  hata watakapomaliza masomo yao watakuwa mabalozi wa kuitangaza vyema serikali na kuwa walipa kodi wazuri.

Ronaldo Adam,amempongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kazi nzuri ya kusimamia suala  ulipaji wa kodi ambazo kwa kweli mchango wake ni mkubwa ambapo  kati ya kazi nzuri ya kukusanya kodi ni ukarabati mkubwa wa majengo katika shule ya Sekondari ya Wavulana Songea.

Alisema, suala la ulipaji kodi sio  jambo la mtu au idara moja ya Serikali, bali kila mtu ana wajibu  na kuhakikisha analipa kodi za Serikali na kuwataka wazazi na jamii kulipa kodi kwa wakati tena bila shuruti.

Ameiomba serikali kupitia Tra kuendelea kutoa elimu  ya kodi kwa jamii juu  na kutumia vyombo  vya habari ili elimu ya ulipaji kodi iwafikie watu wengi,badala ya kujikita zaidi katika maeneo ya mjini ambako watu wengi wameshaelewa maana ya kulipa kodi.

Amemuomba Rais Dkt John Magufuli na wasaidizi wake wa nafasi mbalimbali  katika utumishi wa umma,kufanya kazi usiku na mchana  na kutovunjika moyo kutokana na maneno ya baadhi ya watu wakiwemo wana Siasa uchwara wasioitakia mema nchi yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...