Na Mwaandishi Wetu Mtwara
KIWANDA cha Saruji cha Dangote Mkoani Mtwara kinatarajia kujenga kituo chake cha pili cha gesi asilia (CNG-Compressed Natura Gas) katika mkoa wa Dar es Salaam ambacho kitatumika kutoa gesi safi, salama na kwa gharama ya chini kwa malori yanayosafirisha saruji kwenda sehemu mbalimbali nchini.
Hivi karibu kiwanda hicho kilizindua kituo cha kwanza kilichopo kiwandani Mkoani hapa (Mtwara) chenye uwezo wa Mita za Ujazo 5000 kwa saa (sawa na lita 5000 za mafuta [Automated Gas Oil]). Kituo hicho kitatumika kutoa gesi safi, salama na kwa gharama ya chini kwa takribani malori 250.
Waziri wa Nishati Medard Kaleman alizindua kituo hicho na kuwapongeza uongozi wa kiwanda cha Dangote kwa uwekezaji wa kituo hicho cha CNG.
Akizungumza katika hafla ya kuzindua kituo hicho Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Dangote Engineer Abdullahi Baba alismea malori hayo yamebadilishwa kuweza kutumia mifumo miwili yaani AGO (mafuta) na CNG (gesi asilia) kwa wakati mmoja.
“Pamoja na hayo uwezo, wa kituo hicho utatosha kusaidia katika mkakati wa kampuni juu ya matumizi ya mafuta hapo baadae ambao pia utahusisha matumizi ya gesi asilia katika malori kwa asilimia 100 katika safari zake zote,” alisema.
Akizungumzia kiwanda ambacho kitajengwa Dar es Salaam Baba alisema Kituo hicho kitajengwa jijini Dar es Salaam umbali wa kilomita 550 kutoka kilipo kiwanda cha saruji cha Dangote.
Aliipongeza serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yamevutia kiwanda hicho cha Dangote kuweza kuwekeza kwenye sekta ya gesi huku.
“Kwa mara nyingine tena kiwanda cha Dangote kimefungua njia katika soko kupitia utekelezaji wa teknolojia hii huku kikipata msaada mkubwa kutoka kwa serikali ya Tanzania, na kwa sasa kiwanda cha Dangote kimejipanga kuwa watumiaji wa kubwa wa pili wa gesi asilia nchini baada ya TANESCO,” alisema.
Alisema Tanzania ni kama Nigeria, imejaaliwa akiba kubwa ya gesi asilia ambapo matumizi ya gesi hii katika magari yana manufaa makubwa kifedha na kimazingira.
“Nataka niwahakikishie Dangote na wale wengine wenye nia kutumia rasilimali ya gesi katika magari, serikali ipo pamoja na nyinyi kuhakikisha kwamba inaweka na kujenga mazingira wezeshi ili kaiz yah ii iwe endelevu,” alisema Waziri Kaleman.
Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Dangote Engineer Abdullahi Baba akitoa hotuba katika hafla ya kuzindua kituo chao cha kwanza cha kusindika gesi asilia kwenye mabasi Yao yanayosafirisha Saruji kwenda mikoani
Mtambo wa kusindika gesi asilia kwenye malori
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...