Na Farida Saidy, Morogoro.
WANAWAKE wametajwa kukabiliwa na changamoto mbalimbali kwenye biashara kutokana na kukopa fedha za kuendesha biashara zao kwenye maeneo yasiyo rasmi ya kutoa mikopo, hivyo hulazimika kulipa riba kubwa zaidi na kusababisha kushindwa kuendeleza biashara zao na fedha zote kuishia kwenye kulipa mikopo hiyo.

Hayo yameelezwa na  Meneja bidhaa mwandamizi wa huduma za kibeki Bi. Recho Senni  katika kongamano lililoratibiwa na Bank ya CRDB na kuwakutanisha wajasiliamali wadogo pamoja na vikundi vya wanawake kutoka  Wilaya mbalimbali za Mkoani Morogoro, ambapo ameeleza wanawake wengi wanashindwa kufikia malengo yao kutokana kukopa mikopo isiyo rasmi.

Aidha amewataka Wanawake mkoani humo kuachana na mikopo inayowafilisi badaya ya kuwanufaisha, huku akiwasisitiza wanawake kujiwekea akiba kupitia Malaika Akaunti inayosimamiwa na Bank ya CRDB.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Meneja Biashara  Kanda ya Kati Bi. Jane Maganga amesema lengo la kongamano hilo ni  kuwajengea uwezo wanawake katika namna ya kutunza na kutumia fedha  pamoja na kutoa fursa kwa wanawake katika huduma mbalimbali za kibenki ikiwemo mikopo yenye riba nafuu kwa kina mama.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Loata Ole Sanare amewahimiza wanawake mkoani Morogoro kuunda vikundi vya akina mama, ambapo vitawasaidia kupata Mikopo kiurahisi ikiwemo mikopo inayotolewa na Serikali pamoja na taasisi kibenki.Nao baadhi ya wajasiliamali waliohudhuria kongamano hilo, wamesema elimu waliyoipata imewatoa katika Giza nene na kuishukuru CRDB kwa kuona thamani na mchango wao katika jamii.

Meneja Bidhaa mwandamizi huduma za kibenki kwa wanawake,  Recho Senni akizungumza na wajasiliamali pamoja na vikundi vya kinamama(hawapo pichani) waliofika katika kongamano hilo, katika ukumbi wa Glonecy 88 uliopo Mjini Morogoro.

Baadhi ya washiriki wakiingia ukumbini kwenye ukumbi wa Glonecy 88 Mjini Morogoro,kwenye  kongamano Malikia Akaunti lililoandaliwa na Bank ya CRDB
Meneja Bidhaa Mwandamizi wa Huduma za Kibenki Bi.Jane Maganga akizungumza  kwenye kongamano Hilo wakati akitoa mada mbalimbali na Huduma zinazotolewa na Bank ya CRDB.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika Mstari kwaajili ya kupata chakula kilichoandaliwa na kwenye kongamano Hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Loata Ole Sanare.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...