*AWAONYA WANAOPATA MSAMAHA WA VIFUNGO KUACHA KURUDIA UHALIFU
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka watu wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na uvunjifu wa amani ikiwa pamoja na kuacha kujiingiza tena kwenye matukio ya uhalifu na badala yake wajikite katika kuleta maendeleo kwenye jamii.
IGP Sirro amesema hayo leo wakati akizindua kitabu cha muongozo wa kufichua na kuzuia uhalifu kitabu ambacho kinalenga kutoa dira hasa katika utekelezaji wa mpango wa Polisi kata kupitia mpango mkakati wa ushirikishwaji wa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...