Katika taarifa iliyotolewa na Mtaalamu wa Masuala ya Mawasiliano kutoka Mfuko wa Ubunifu wa Mendeleo ya Watu (HDIF), Hannah Mwandoloma iliyotolewa leo Mei, 11, 2021 imesema kuwa maonesho hayo yataanza Mei 17-22, 2021 jijini Dar es Salaam.
Kaika maonesho hayo wadau mbalimbali wa ubunifu watajumuika pamoja wakiwemo mashirika binafsi, wadau wa maendeleo, watunga sera, wataalam mbalimbali, wasomi pamoja na wabunifu ili kujadiliana na kubadilishana ujuzi kuhusiana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosema “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na Jumuishi”
Kwa Dar es Salaam wiki hiyo itafanyika katika kumbi za LAPF Tower, Makumbusho.
Taarifa hiyo imewaomba wadau wote wa ubunifu wanaaswa kujitokeza kwa wingi kwenye maonyesho hayo ili kujadili mijadala mbali mbali ambayo pia itarushwa kwa njia ya redio, runinga na mitandao ya kijamii.
Wiki ya Ubunifu Tanzania imeandaliwa UKaid kupitia Mfuko wa Ubunifu wa Mendeleo ya Watu (HDIF), kwa ushirikiano na Costech na UNDP, wadau mbalimbali kwa udhamini mkubwa wa Vodacom, NMB Bank, European Union, UNCDF, Tigo, Ubalozi wa Netherlands, CRDB Bank, UNICEF, Segal Family Foundation, Ubalozi wa Uswizi, Ifakara Innovation Hub na UNWomen.
Unakumbushwa kuzingatia umbali kati yako na mwingine, kunawa mikono, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...