USHINDI lazima! Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Aesh Hilaly amesema ushindi wa chama hicho kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge utakaofanyika Jumapili ya Mei 16 hauepukiki.
Aesh ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa CCM katika kikao cha ndani pamoja na wafanyabiashara wa Soko la Buhigwe alipofika wilayani hapo pamoja na wabunge wenzake kumuombea kura mgombea Ubunge wa CCM, Kavejuru Felix.
“ Tumekuja kushiriki kampeni hizi sisi kama wabunge ili kuhakikisha Chama chetu kinapata ushindi mkubwa katika uchaguzi huu mdogo, lengo letu ni kuwaonesha wapinzani kwamba imani iliyopo kwa wananchi kwetu ni kubwa na wanahitaji kuletea maendeleo na serikali ya CCM.
Watu wa Buhigwe mmepata heshima kubwa sana ya kuwa na Makamu wa Rais hii ni imani kubwa hivyo niwaombe kama mlivyompa Dk Mpango kura nyingi katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2020 basi mkampatie kura za kishindo pia ndugu yetu Kavejuru Mei 16 ili ashirikiane na Rais Samia na Makamu wa Rais Dk Mpango katika kutekeleza miradi ya maendeleo jimboni kwetu,” Amesema Aesh.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...