Na Mohamed Samli, Michuzi TV

RAIA 29 wa Burundi wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam wakikabiliwa na  shtaka moja la kuingia katika jamhuri ya muuungano wa Tanzania bila ya kuwa na vibali maalumu.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali kutoka Idara ya Uhamiaji Godfrey Gwilo amedai mbele ya hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa, Mei 25 mwaka huu, huko  Kariakoo ndani ya Wilaya  ya Ilala jijini Dar es salaam washtakiwa waliingia nchini kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo washtakiwa 13 walikana kosa hilo na kudai kuwa wana vibali maalumu na wengine 16 walikubaliana na tuhuma hizo na kujibu kuwa ni kweli.

Hakimu amewataka washtakiwa wote walio jitetea si kweli wafike na vibali  vyao (documents) zitakazo onesha kuwa wana uhalali wa kuishi  nchini. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni Mosi mwaka huu, washtakiwa  wote wamerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...