Smart Codes ilianzishwa mwaka 2010 na Ndg. Edwin Bruno. Kampuni ilisajiliwa mwaka 2014 kama kampuni yenye kikomo na kila siku inazidi kukua. Katika muda wote huu, lengo kubwa la kampuni limekuwa ni kuleta mabadiliko ya kidigitali kwa wateja na washirika wetu. Hiki hakitabadilika kwa sababu kampuni ina matarajio ya kufanya makubwa zaidi katika mwongozo huu.
“Kuanzishwa kwa SAG kunawezesha kampuni kusimamia ukuaji na kuongeza Imani kwa wateja wetu. Kazi kubwa ya SAG ni kushauri, kuongoza na kuweka dira. Itasimamia utendaji na kuwa maono ya pamoja miongoni mwa kampuni tanzu ili kusaidia kulinda matarajio ya wateja, na pia kuhakikisha kwamba kila kampuni tanzu inaendelea kukua katika kiwango kilichowekwa na Smart Codes hapo kabla. Kwa kuunda SAG, tunawahakikishia washirika wetu kwamba tuna timu bora, mbinu sahihi na taratibu zenye umakini” alisema Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.
Kampuni hizi tanzu 5 zinajumuisha; Smart Codes ambayo inatoa huduma za matagazo na masoko zilizo kamilifu zinazojumuisha upangaji mbinu,huduma za kidigitali, ubunifu, media,shughuli/hafla, hamasa za hadhara na uhusiano kwa umma; Smart lab itaendelea kuwa maabara ya uvumbuzi na kuchochea ubunifu ikihusiana na programu, ujuzi, vipaji na maabara za kuchochea ubunifu; Smart Foundry inahusiana na uundaji wa bidhaa kuanzia utengenezaji wa mbinu, ubunifu, maendeleo na usimamizi; Smart Nology inahusika zaidi na teknolijia katika huduma zetu wenyewe kwa kutoa nyenzo za kutengenezea tovuti, njia za malipo, aplikesheni za simu mpaka kwenye uundaji wa aplikesheni za bahati nasibu; na Smart Studio inatoa huduma za utengenezaji picha na sauti na pia picha za uhuhishaji (animation.)
“Lengo kubwa la SAG ni kutengeneza jukwaa litakalowezesha kushirikiana na kampuni za kiafrika katika kuacha alama kupitia teknolojia, media na ubunifu. Haya yote yatawezeshwa na kampuni zetu tanzu 5 zitakazofanya kazi kubwa ya kuhakikisha washirika wetu wanakabiliana kwa usahihi na changamoto zao. Tunaungana na kampuni na chapa za kiafrika zenye lengo la kuleta mapinduzi ya kidigitali. Kama methali ya kiafrika inayosema, “kama unataka kwenda haraka nenda mwenye, kama unataka kwenda mbali nenda na wenzako” alimalizia Ndg. Edwin Bruno, CEO na CVO wa SAG.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...