Mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu, George Mkangala kushoto akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa viongozi wa mtaa wa kata ya Msongola jimbo la Ukonga wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar Es Salaam kuhusu mafunzo ya kuijua sheria ya kazi na Ajira. Kulia ni aliyesimama ni Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Rodger Michael.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Msongola, Luhungu Renatus akizungumza na viongozi wa serikali za Mtaa wa kata ya Msongola wakati Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake wakitoa mafunzo ya kuijua sheria ya kazi na Ajira.
Viongozi mbalimbali wa serikali za mtaa na wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mafunzo ya kuijua sheria ya kazi na ajira iliyotolewa na kituo cha Msaada wa Kisheria kwa wanawake(WLAC).
Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Rodger Michael akifafanua jambo katika mafunzo ya ufahamu wa masuala ya sheria za kazi na Ajira. katika Mafunzo yaliyofanyika katika Kata ya Msongola iliyopo jimbo la Ukonga wilaya ya Temeka mkoa wa Dar es Salaam.
Afisa Maendeleo ya jamii,  Theodora Kavishe akizungumza wakati wa mafunzo ya kuijua sheria ya kazi na Ajira iliyotolewa na Kituoc cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC) katika Kata ya Msongola Jimbo la Ukongo wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

KITUO Cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake(WLAC)katika kuendelea kutatua migogoro kati ya waajiri na waajiriwa leo wametoa elimu juu ya sheria ya kazi na ajira kwa viongozi wa Kata ya Msongola jimbo la Ukonga wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kutoa elimu juu ya sheria ya ajira na kazi, mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu, George Mkangala, amesema kuwa wafanyakazi wanawake na wanaume wanahaki sawa ya ujira na kazi inayofanana.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuondoa migogoro ambayo ipo kati ya waajiri na waajiriwa kwani kila mmoja akijua haki na wajibu wake na akizingatia migogoro ya waajiri na waajiriwa haita kuwepo au itapungua.

Mkangala amesema kuwa sheria ya ajira na mahusiano kaini ya 2004 katika kifungu namba Saba (7) kimeainisha haki ya mfanyakazi  kutokubaguliwa katika sehemu ya kazi kwa namna yeyote ile iwe kwa misingi ya rangi, kabila, uaifa, sehemu ya kuzaliwa, uraia mtazamo wa kijinsia, kisiasa, hali ya ujauzito na hali ya ulemavu.

"Hivyo jamii ielewe sheria ya ajira na kufanya kama sheria inavyosema na sio vinginevyo, ikiwa mtu akitendewa tofauti na sheria ya ajira na kazi inavyosema inaweza kutatuliwa katika mabaraza ya usuluhishi kati ya mwajiriwa na mwajiri." 

"Kufanya Kazi bila mkataba kunahatari kadhaa panapokosekana ushahidi wa kisheria kuwa umeajiriwa na itakuwa rahisi kupoteza haki zako za msingi wakati wowote kutakapotokea shauri au mgogoro kati ya mwajiriwa na mwajiri." Amesema Mkangala.

Hata hivyo ameshauri jamii kuwa mkataba wa kazi wa maandishi ndio bora zaidi kwani unaweka kumbukumbu sawa kwa mwajiriwa na mwajiri.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kata ya Msongola, Luhungu Renatus amewapongeza WLAC kwa kuwafikia wakazi wa Kata ya Msongola, pia ameomba wadau wengine wa maendeleo wanaotoa elimu mbalimbali wawafikie kata hiyo na wao wapo teyari kupokea mafunzo mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya jamii nzima ya kata ya Msongola.

Mradi wa Kuiwezesha jamii kuijua sheria ya kazi na ajira ambao unatekelezwa kwa miaka miaka miwili ingawa kwa wanaenda kutamatisha mwaka huku wakiwa wametembelea baadhi ya kata za mkoa wa Dar es Salaam.

Viongozi wa Kata ya Msongola waliopata mafunzo hayo ni maafisa watendaji, viongozi wa serikali za mtaa, maafisa maendeleo pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...