Na Karama Kenyunko Michuzi TV
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu ya kesi ya uchochezi iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Freeman Mbowe na wenzake na kuamuru warejeshewe kiasi cha sh. Milioni 350 walicholipa kama faini mwaka 2020.

Uamuzi huo umetolewa na Jaji Irvin Mgeta leo Juni 25,2021.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Mgeta amesema ameangalia na kuzingatia kuwa hukumu iliyotolewa ilikuwa na mapungufu ya uchambuzi wa ushahidi na kwamba washtakiwa hawakuwa na kosa na hivyo anawaachia huru.

Akifafanua kosa la 2,3,4 ambayo ni ya kufanya mkusanyiko isivyo halali, kuandamana bila kibali na kukiuka amri ya polisi ya kuwataka kuacha kuandamana, Jaji Mgeta amesema, katika uchambuzi wake ameona eneo la Buibui

ambalo washtakiwa walidaiwa kutenda kosa, lilikuwa eneo halali kwa mkutano wa kampeni hakuna ushahidi unaonyesha nini kilitendeka pale isipokuwa wengi wa mashahidi walikuwa wakizugumzia barabara ya Kawawa.

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ni pamoja na mkanda wa video, lakini katika video ile ilionyesha watu wa alikuwa wakiandamana kwa amani huku wakiwa wamenyoosha mikono juu lakini jeshi la polisi ndio lilianzisha vurugu baada ya kuanza kulipuwa mabomu ya machozi ili kutawanya watu.

Akifanua juu ya mashtaka ya uchochezi, Jaji Mgeta amesema, mashtaka hayo yalikuwa na mapungufu, hati ya mashtaka pia ilikuwa na mapungufu kwa sababu haikuanisha ni Makundi gani yaliyochochewa na kuathirika.

"Wakati wa uchaguzi wanasiasa hutumia maneno mbali mbali kwenye majukwaa ili kunadi sera zao..., kesi ambayo Hakimu wa Mahakama ya Kisutu (Thomas Simba) aliitumia ya Hussein Kasanga dhidi ya Jamuhuri ilitolewa mwaka 1974 wakati wa chama kimoja", amesema Mgeta.

Amesema katika kesi hii ya Mbowe na wenzake huwezi kusema walifanya chuki dhidi ya nani lakini katika kesi hiyo inaonyesha Kasanga alisambaza chuki dhidi ya Nyerere ma Chama cha TANU lakini kesi ya Mbowe na wenzake pia imetunguliwa wakati wa mfumo wa vyama vingi hivyo lazima kuwe na lugha za kuhamasisha wananchi juu ya chama husika.

"Nimeona mashtaka yote dhidi ya washtakiwa yalikuwa hayajathibitishwa hivyo nawaachia huru. Aidha Jaji Mgeta amesema licha ya kwamba Vincent Mashinji alikuwa hajakata rufaa na wenzake lakini moja kwa moja nae anafaidika na rufaa hii hivyo nae arejeshewe fedha zake.

Kesi Hiyo ya 2018 Mbowe na wenzake walikuwa na mashtaka matatu likiwemo la uchochezi na kuandamana bila kibali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...