
EWURA:Soko la mafuta inategemea na soko la dunia.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
KUPANDA kwa bei ya mafuta au kushuka haiwezi kutabiliwa kutokana na soko la dunia.
Hayo amesema Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo wakati Maonesho ya 45 ya Biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.amesema kwa hawawezi kutabiri Mafuta kwa mwezi unaofuata kutokana na soko hilo kushindwa kutabilika na sio Tanzania Duniani kote.
Amesema EWURA wanapopanga bei elekezi wanakuwa wameshajiridhisha katika soko la ndani bila kumuathiri muuzaji wa jumla pamoja na yule wa Kati kwenda kwa watumiaji wa Nishati hiyo.
Aidha amesema pasipo kuwepo na udhibiti kungekuwa na mfumuko wa bei na kufanya maisha kupanda kutokana na asilimia 95 inategemea nishati hiyo.
Kaguo amesema kuwa udhibiti katika ukaguzi unafanyika kila mara ili kufanya baadhi ya watu wasipandishe bei ya nishati ya Mafuta.
"Tumekuwa tunafatilia kwa ukaribu watoa huduma wa nishati ya Mafuta na wanaokiuka kwa kupandisha bei wanachukuliwa hatua pamoja na kufuta leseni za utoaji huduma."Amesema Kaguo.
Aidha amesema kuwa Mafuta kupanda kutokana na kupanda kwa dola ambayo hakuna mtu anaweza kujua dola itapanda au itashuka kwa mwezi unaofuata.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...