MSHTAKIWA Frank Mahelela, anayeishi mkoani Dar es Salaam amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la wizi wa zaidi ya sh. Milioni 300 na kujifanya yeye ni afisa wa Benki.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, Ester Martin mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Ritha Tarimo imedai kati ya Mei ,28, 2019 na Septemba 30, 2019 katika maeneo la Taasisi ya Kimataifa ya Wahamiaji (nternationa Organization for migration), iliyopo Masaki Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa Mahelela akiwa Mhasibu wa taasisi hiyo, aliiba USD 156,000 ambazo sawa na Sh
Milioni 358 fedha ambazo zilikuja mikononi mwake kupitia nafasi yake kazini.
Katika shtaka la pili imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa huyo alighushi kadi ya mpiga kura yenye jina la Airi Asalaam kwa kujifanya kwamba kadi hiyo ni halali na imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
Imeendelea kudaiwa kuwa, Mei 28, 2019 huko katika benki ya Azania Tawi la Masdow, mshtakiwa kwa nia ya kudanganya aliwasilisha kitambulisho hicho kwa Afisa huduma wa benki hito, Wahida Abubakari Jambya akidai kuwa kilikuwa ni nyaraka halalali na imetolewa na (NEC).
Aidha, Mei 28, 2019 mshtakiwa Mahelela kwa ndia ya kudanganya alijitambulisha katika benki hiyo ya Azania kuwa yeye ni Airi Asa Salaam kwa Wahida Jambya, kitu ambacho sio kweli.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa mahabusu hadi kesho, Julai 29,2021 kesi hiyo utakapokuja kwa ajili ya mshtakiwa kukamilisha taratibu za dhamana.
Mshtakiwa Frank Mahelela akiingi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...