Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KLABU ya Yanga imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Watani wao wa Jadi, Simba SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa ukishududiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyefanya ‘surprise’ kwa Mashabiki wa Soka waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.
Bao pekee la Yanga SC lilifungwa na Kiungo wa Klabu hiyo, Zawadi Mauya dakika ya 11 ya mchezo baada ya kupiga shuti kali lililomgonga Beki wa Simba SC, Shomari Kapombe na kutinga wavuni likiwaacha Simba wakishangaa dakika za mwazo za mchezo huo.
Yanga SC walionekana kuzuia kwa kuwa wengi golini kwao dakika zote huku wakitumia mchezo wa kushambulia kwa kushtukiza (Counter Attack) licha ya ubora wa Mabeki wa Simba SC, wakiongozwa na Sergio Pascal Wawa, Joash Onyango na wengine Shomari Kapombe, Mohammed Hussein.
Mabeki wa pembeni wa Yanga SC, Kibwana Shomari na Adeyum Salehe walionekana kumbana vilivyo Mchezaji msumbufu wa Simba SC, Bernard Morrison na kukosa nafasi ya kufurukuta katika mchezo huo licha ya ubora wa safu ya Kiungo kikiongozwa na Clatous Chama.
Simba SC imeshindwa kutangaza Ubingwa wa Ligi Kuu Bara (VPL) mbele ya Yanga SC sasa itasubiri michezo yake iliyobaki katika Ligi hiyo dhidi ya Azam FC, Namungo FC, Coastal Union na KMC FC.
Katika msimamo wa Ligi hiyo, Simba SC bado wanaongoza Ligi wakiwa na alama 73 na michezo 30 wakati Yanga SC wakiwa na alama 70 wakiwa na michezo 32.
Timu hizo zitakutana tena katika Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Julai 25, 2021 katika dimba la Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...