Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) nchini imeaswa kufanya jitihada za ziada katika kuyaongezea thamani mazao ili kuweza kushindana na soko la nchi za nje.
Hayo yalisemwa na waziri wa kilimo Mhe. Profesa Adolf Mkenda wakati akizindua viwanda vya bodi hiyo ya mazao mchanganyiko vilivyozinduliwa mnamo Jumatano iliyopita katika makao makuu ya Tanzania jijini Dodoma.
Profesa Mkenda aliitaka bodi hiyo na sekta binafsi zinazojihusisha na uchakataji wa mazao nchini kuhakikisha wanaongeza thamani ya mazao ili kuweza kuyapeleka kuuza nchi za nje.
Alisema kuwa ni vyema bodi hiyo ikaangalia ni namna inaweza kushirikiana na wakulima katika kuyaongezea thamani mazao.
“Nyie bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko mkisaidia na sekta binafsi mnaweza kutusaidia kuhakikisha mazao yetu yanaongezewa thamani,” alisema Profesa Mkenda.
Pia alitoa wito kwa bodi hiyo kuhakikisha inaingia mikataba na wakulima wenye mashamba makubwa nchini ili waweze kulima alizeti ya kutosha.
Naye Mkurugenzi wa bodi hiyo Bw. Anselm Moshi alisema kuwa kiwanda hicho cha alizeti kinauwezo wa kuchakata tani 40 kwa siku kutokana na ugumu wa upatikanaji wa malighafi.
“Kwa kuona hitaji la kuwa na mafuta yenye ubora, maana kuna mafuta mengi ya alizeti yanayochakatwa mitaani ambayo hayana ubora unaotakiwa, na hivyo viwanda hivi vitakuwa ni suluhisho la changamoto hiyo ya ubora,” alisema Bw. Moshi.
Aidha, naye Mbunge wa Dodoma Mjini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema kuwa viwanda hivyo vitakuwa mkombozi kwa wakulima nchini.
“Zaidi ya watu 6500 watanufaika na viwanda hivi na hasa tukiongeza utaratibu wa kuwapa mikataba wakulima wetu wakawa ni wazambazaji wakuu wa malighafi tutakuwa pia tumeisaidia sana serikali katika kupunguza tatizo la ajira nchini,” alisema Mhe. Mavunde.
Waziri
wa Kilimo nchini Mhe. Profesa Adolf Mkenda (wapili kushoto)
akishirikiana na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde, Mkurugenzi
wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko (CPB) Dkt. Anselm Moshi na viongozi
wengineo kuzindua viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano
iliyopita.
Waziri
wa Kilimo nchini Mhe. Profesa Adolf Mkenda akipokea maelezo ya bidhaa
itokanayo na zao la alizeti wakati wa sherehe ya kuzindua viwanda vya
uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.
Waziri
wa Kilimo nchini Mhe. Profesa Adolf Mkenda akipokea maelezo juu ya
mafuta yatokanayo na zao la alizeti wakati wa sherehe ya kuzindua
viwanda vya uchakataji mazao jijini Dodoma Jumatano iliyopita.
DO YOU NEED A PERSONAL/BUSINESS/INVESTMENT LOAN? CONTACT US TODAY VIA WhatsApp +19292227023 Email drbenjaminfinance@gmail.com
ReplyDeleteHELLO
Loan Offer Alert For Everyone! Are you financially down and you need an urgent credit/financial assistance? Or are you in need of a loan to start-up/increase your business or buy your dream house. Are you in search of a legit loan? Tired of Seeking Loans and Mortgages? Have you been turned down by your banks? Have you also been scammed once? Have you lost money to scammers or to Binary Options and Cryptocurrency Trading, We will help you recover your lost money and stolen bitcoin by our security FinanceRecovery Team 100% secured, If you are in financial pains consider your financial trauma over. We Offer LOANS from $3,000.00 Min. to $30,000,000.00 Max. at 2% interest rate NO MATTER YOUR CREDIT SCORE. GET YOUR INSTANT LOAN APPROVAL 100% GUARANTEED TODAY VIA WhatsApp:+19292227023 Email: drbenjaminfinance@gmail.com