Na Mwandishi wetu, Hanang'
Hanang’.
MASHINDANO ya Mount Hanang’ Cup yanatimua vumbi Wilayani Hanang’ Mkoani
Manyara, yakihusisha michuano ya kandanda, riadha na mpira wa pete.
Mbunge
wa jimbo la Hanang’ mhandisi Samwel Hhayuma amesema mashindano hayo ya
kutangaza mlima Hanang’ unaoshika nafasi ya nne kwa urefu hapa nchini
yatachangia kuibua vipaji vipya vya wanamichezo mbalimbali wa soka,
riadha na mpira wa pete.
Mhandisi
Hhayuma amesema mashindano hayo yatahusisha wanamichezo chipukizi wa
riadha, soka na pete kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vyao ili
wafike mbali ikiwemo ngazi ya kimataifa.
Amesema
kuanzishwa kwa michezo hiyo mbalimbali kutasaidia kuinua vipaji na
kuweza kuiwakilisha nchi katika mashindano makubwa kama Olimpiki na
kuhamasisha wananchi kutembelea mlima Hanang’.
“Tumeita
michuano hii Mount Hanang’ Cup kwa ajili ya kuutanga mlima wetu na pia
tunataria tutapiga hatua kimichezo na wanamichezo kupata fursa ya
mashindano haya,” amesema mhandisi Hhayuma.
Amesema
michezo hiyo itakuwa inafanyika kila mwaka hivyo wachezaji chipukizi
watapita hatua kubwa japokuwa michezo ina changamoto mbalimbali ila
kupitia wadau watafanikisha kufika mbali.
Amewahimiza
wananchi wa eneo hilo kushiriki michuano hiyo kwa kufika kwa wingi ili
kupata burudani na kupata taarifa mbalimbali za mlima Hanang’.
Mmoja
wa wafanyakazi kwenye hifadhi ya mlima Hanang’ John Masatu amesema
watatumia michezo hiyo kukuza utalii wa ndani kwa wananchi wa Hanang’
mkoa wa Manyara na Taifa kwa ujumla ili kuongeza kipato cha nchi.
“Mlima
Hanang’ una msitu mzuri mno, maporomoko ya maji na vivutio mbalimbali
vinavyowafaa watu kupumzika hivyo kupitia mashindano haya vijana
watakuza vipaji na kutangaza mlima wetu,” amesema Masatu.
Amesema
wanamichezo mbalimbali wa hapa nchini, wakiwemo wa timu za Simba, Yanga
na Azam, wanapaswa kufika Hanang’ kwa ajili ya kutembelea na kufanya
mazoezi kwani hali ya hewa ya eneo hilo inaruhusu.
Mchezaji
wa timu ya soka ya Endasak, Mathew Bayo amempongeza mhandisi Hhayuma
kwa kuandaa michuano hiyo ambayo kwa namna moja au nyingine itakuza
vipaji vya eneo hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...