Charles James, Michuzi TV

UJENZI wa Maabara changamano katika Tume ya nguvu ya Atomiki upo katika awamu ya pili ambapo itakua na maabara nane na kituo cha usalama wa mionzi na kinga.

Mradi huo unafanywa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambapo ujenzi huo umegawanyika katika awamu mbili na mpaka sasa umefikia asilimia 85.

Akizungumza na wandishi wa habari ambao wamefika katika eneo hilo kujionea maendeleo ya ujenzi huo, Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Edgar Mbaganile amesema awamu ya kwanza ya mradi huo una maabara nne zinazofanya kazi na ulianza kujengwa mwaka 2017 huku ukiigharimu Serikali kiasi cha Sh Bilioni 2.3.

Amesema baada ya kukamilika kwa mradi huo waliingia mkataba wa pili na TBA wenye thamani ya Sh Bilioni 10.4 na mpaka sasa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeshawapatia Sh Bilioni 6.1 kwa ajili ya ujenzi huo.

" Huu ni mradi wa awamu ya pili ambao ukikamilika utakua na maabara nane za kisasa na kituo cha mafunzo ya usalama na kinga ya mionzi, Amesema Mbaganile.

Amesema Atomiki ni mionzi ambayo ina manufaa makubwa ambapo hata katika Hospitali teknolojia hiyo inatumika kugundua magonjwa hasa kwenye picha za X-ray lakini pia katika tiba za magonjwa kama Saratani.

"Mradi huu utakua na manufaa makubwa kwa Nchi kwani itaongeza uwezo wa kudhibiti matumizi salama ya mionzi pamoja na kuweka mazingira salama, lakini pia utawezesha kuwa na kituo cha mafunzo kwani wataalamu walikua wachache hivyo itaongeza idadi ya wataalamu na wananchi wataweza kupata huduma," Amesema Mbaganile.

Muonekano wa mradi wa ujenzi wa maabara changamano katika Nguvu za Atomiki awamu ya pili ukiwa unaendelea katika eneo la Njiro jijini Arusha. Mradi huo unafanywa na Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.
Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), Edgar Mbaganile akizungumza na wandishi wa habari kuelezea mradi huo unaotekelezwa wa maabara changamano katika Tume hiyo.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutembelea Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) kujionea ujenzi wa maabara changamano katika Tume hiyo unaotekelezwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

 Mkurugenzi wa Huduma za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania TAEC, Edgar Mbaganile (mwenye koti jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na wandishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini waliofika kutembelea Tume hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...