Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM ), Wilaya ya Bagamoyo ,mkoani Pwani, kimeiagiza
ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo na watendaji wake
,kuhakikisha wanatolea majibu na kutatua changamoto za muda mrefu
zinazotolewa na madiwani bila majibu.
Aidha
kimetaka wataalamu kushirikiana na madiwani na kujenga mahusiano mazuri
ili kuimarisha mahusiano mazuri katika utendaji kazi wao.
Katibu
wa CCM Bagamoyo, Getruda Sinyinza alitoa maagizo hayo wakati wa kikao
Cha madiwani Bagamoyo,Chenye ajenda kuu kuwasilisha taarifa za kata kwa
kata.
Alisema ,zipo
changamoto ambazo zipo ndani ya uwezo wa Halmashauri na wataalamu ambazo
zinapaswa kutekelezwa kwa haraka pasipo kukaa nazo na kujikumbusha kila
kikao kwa kipindi kirefu .
"Madiwani
hawa wanatoa taarifa hizi kutoka kwa wananchi ,,hawazitoi kichwani mwao
, hivyo zinahitaji matokeo ,;"Ili tunusuru wananchi hawa tunaomba mambo
yote mkayafanyie kazi ,na changamoto zisizo na majibu zisemwe pasipo
kukaa kimya" alifafanua Getruda.
Kwa
upande wake ,mwenezi wa Wilaya (CCM) ,John Fransis Bolizozo aliwaasa ,
watumishi na watendaji wapige kazi waache kufanya kazi kwa mazoea .
"Tufanyeni
kazi ,tunamsaidie Rais na mwenyekiti wetu wa CCM Taifa ,Samia Suluhu
kuyaeleza yote yanayofanywa na serikali na ambayo yapo katika hatua za
utekelezaji ili kuondoa maswali kwa jamii.'"alibainisha Bolizozo.
Nae
mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo , Mohammed Usinga
akipokea maelekezo hayo ,alimtaka mkurugenzi na timu yake kupeleka
watumishi wa kukusanya mapato katika chanzo Cha mchanga na mazao ya
matunda kata ya Fukayosi.
Alieleza,
halmashauri ipo kwa ajili ya kulenga kuongeza mapato ,hajaridhishwa
kusikia kuna changamoto ya ukosefu wa watumishi hao .
Usinga
pia alielekeza ,, mkurugenzi na Bwana fedha kuhakikisha fedha asilimia
10 ,fedha za vibarua na za wazabuni wa makusanyo zinapelekwa kwa wakati.
"Wanatufanyia
kazi nzuri ,kwenye wastani wa milioni kumi sasa tumefikia zaidi ya
milioni 20,tusicheleweshe fedha zao itasababisha upenyo wa wizi"anasema
Usinga.
Awali
,akiwakilishwa diwani wa Fukayosi,Ally Ally Issa taarifa yake ya kata
,imeweka bayana tatizo la ukosefu wa watumishi wa kukusanya mapato
kwenye chanzo Cha mchanga na mazao ya matunda.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...