Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo


MKUU wa Wilaya ya Bagamoyo,Zainab Abdallah ameagiza mtumishi atakaebainika kutumia fedha mbichi za makusanyo ya mapato kwa manufaa ya tumbo lake ,ashughulikiwe ili iwe fundisho .

Aidha ameelekeza ,kuboresha na kuibua vyanzo vipya ili kuinua mapato kutoka asilimia 93 ya sasa hadi kuvuka asilimia 100 na inawezekana.

Akizungumzia maagizo kutoka kwa waziri wa TAMISEMI kuhusu masuala ya kudhibiti mapato na upotevu wa fedha , Zainab ameshuka chini nae kutoa maagizo kupitia baraza la madiwani la halmashauri hiyo .

Mkuu huyo wa Wilaya alieleza, haiwezekani mtumishi abainike kufanya ubadhilifu pasipo kuchukuliwa hatua stahiki ,"Nawaomba madiwani msimamie hili hali itakayosaidia kukomesha tabia hii."

"Kuanzia Sasa hakuna kuchukua fedha kwa wakusanyaji kabla ya makusanyo kufikishwa bank na kwenye mfumo ndipo itolewee kwa taratibu zinazotakiwa "

Alieleza, mwaka Jana kulikusanywa bilioni 3.2 sawa na asilimia 93 hivyo iongezwe nguvu ili kupata makusanyo makubwa.

"Pia makusanyo sekta ya utalii hatupo vizurii sana ,nitahakikisha na mkurugenzi tunasimamia eneo hili pia kuinua mapato "alisisitiza Zainab.

Hata hivyo ,alitaka madiwani wasimamie fedha za miradi kuhakikisha zinafika katika maeneo lengwa ikemo asilimia 10 inayotengwa kwa ajili ya vijana,wanawake na walemavu ili kudhibiti vikundi hewa.

Pamoja na hayo, Zainab amejipanga kufanya kikao na wadau wa maendeleo ,na aliomba ushirikiano wa wadau na wawekezaji kusaidia kutatua changamoto mbalimbali .

Alisema Wilaya imepokea bilioni moja kwa Bagamoyo na bilioni moja nyingine kwa ajili ya Chalinze kutoka Serikalini kwa ajili ya matengenezo na maboresho ya barabara za ndani.

Pia wamepokea milioni 500 zinalozotokana na tozo za mihamala ya simu zitakazotumika katika ujenzi wa vituo vya afya .

Mwenyekiti wa halmashauri ya Bagamoyo, Mohammed Usinga alisema mpango mkakati ni kudhibiti mianya ya wizi kwenye maeneo ya vyanzo vya ndani na kupeleka watumishi wa kukusanya katika maeneo yenye ukosefu.

Alieleza,ushirikiano mkubwa anaoutoa mkuu wa Wilaya na mkurugenzi kwasasa unaonyesha ujio wa Bagamoyo mpya na kuwa mji wa mfano.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...