Na Mwandishi Wetu,Michuzi TV
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene, ametoa maelekeza kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama nchini kuwatafuta watu wote wanaowachafua wenzao mitandaoni hasa wanaomdhihaki Rais wa Tanzania na Serikali na hatua kali zifuatwe na kuwafikisha mahakamani kwa haraka.
Ametoa maelekezo hayo leo Septemba 16,2021 Mjini Dodoma wakati akizungimza na viongozi wa idara zote za ulinzi na usalama nchini ambapo ameelekeza kufanyike msako wa haraka kuwabaini watu hao na kuwakamata.
"Kumeibuka tabia ya watu kutumia vibaya mitandaoni ya kijamii kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza,"amesema Waziri Simbachawene huku akisisitiza msako wa kubaini watu hao uanze haraka na kisha sheria ichukue mkondo wake.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene ameagiza msako wa wezi mitandaoni kwa kuwa inakadiriwa kuwa kwa siku milioni 500 zinakua kwenye wizi wa kimatandao huku akikataza wananchi kutoa fedha kwa ajili yakufuatilia Polisi taarifa za simu zao zilizoibiwa.
Home
HABARI
WAZIRI SIMBACHAWENE AAGIZA WANAOMDHIHAKI RAIS,VIONGOZI MITANDAONI WATAFUTWE,WACHUKULIWE HATUA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...