Na Humphrey Shao, Michuzi Tv

WASANII Bwana! Noma sana eti Msanii wa Muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongo fleva kutoka Lebo ya Too Much Money Whozu anauliza hivi Vunjabei na Jokate Mwegelo ni mtu na Shem?

Leo wasanii wanaoshabikia Klabu ya Simba wamekutana katika duka la mfanyabiashata Fred Vunja bei ambaye ameingia mkataba na Klabu hiyo kuuza jezi na vifaa vya michezo.Hivyo wasanii hao ambao wapo kwa Vunjabei akiwemo Darasa wanatumia sanaa zao kutoa burudani kuelekea Simba Day.

Whozu kama ilivyokawaida yake alimua kubadilisha mistari ya wimbo wake wa Ahh Wapi kwa kuwatuliza wasanii  na mashabiki wa simba waliokusanyika katika viunga vya Sinza Kijiweni.Katika mashairi hayo msanii anauliza ; "Vunjabei na Jokate eti ni mtu na Shem" watu na kuitikia Ahh Wapi.

Hakuishia hapo Whozzu akauliza tena hivi Hamisa Mobeto na Vunjabei ni Mtu na Shem ? Majibu ya waliokuwa wanaitikia wanajibu Aah Wapi.Ukweli kwenye eneo hilo wameendelea kutoa kila aina ya burudani.Alitumia sanaa yake kutaja watu kadhaa maarufu.

Wakati huo huo Msanii na Mtangazaji maarufu Beny Kinyaia ametumia nafasi hiyo kuonesha mapenzi yake kwa Klabu ya Simba na wakati ameshika kipaza sauti aliamua kutangaza mpira kwa kutaja wachezaji wa timu ya Simba.

Pamoja na mambo mengine yaliyoendelea katika eneo la Sinza kwenye duka la Vunjabei , idadi kubwa ya wasanii wanaoshabikia Simba wamejitokeza kwa wingi,hali iliyosababisha eneo hilo kufurika mamia ya wananchi waliokuwa wakifuatilia kila kinachoendelea .


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...