BENKI ya Mwalimu (Mwalimu Commercial Bank Plc) imeishukuru Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa hatua zake za kukabiliana na madhara yatokanayo na ugonjwa wa Uviko-19 kwani zilisaidia sekta ya mabenki kuimarika na kuendelea kutoa huduma kuhakikisha uchumi wa  nchi hautetereki.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc, Bw.Francis C. Ramadhani wakati akitoa Taarifa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Tano wa Wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha leo Ijumaa Oktoba 22, 2021.

Alisema Takwimu za Benki Kuu za mwaka 2020 zinaonyesha uchumi wa Tanzania ulikua kwa asilimia 4.7 na unategemewa kukua kwa asilimia 6 katika mwaka 2021 na hii inaonyesha kuimarika kwa sekta mbalimbali za uchumi baada ya janga la UVIKO-19.

“Kwa upande mwingine mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 3.5 hii pia inadhihirisha uwepo wa mazingira mazuri ya biashara.” Alifafanua Bw.Ramadhani.

Akizungumzia mafanikio ambayo benki ya Mwalimu  imepata katika mwaka 2020 Bw. Ramadhani alisema benki hiyo iliingia makubaliano na taasisi tatu kubwa ambazo zinamiliki hisa katika benki yaani Chama Cha Waalimu Tanzania (CWT), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ambao kwa pamoja  walitoa kiasi cha fedha za kitanzania shilingi bilioni 25 ikiwa ni fedha za kuonhgeza amana za kufanya biashara.

“Kwakweli fedha hizi ndugu wanahisa zimeiwezesha benki yetu kuongeza kasi ya utoaji mikopo kwa wateja wetu. Alifafanua." Alisema Mwenyekiti huyo wa Bodi. 

Alisema katika kipindi cha kuanzia Oktoba 2020 hadi Septemba 2021 ambapo jumla ya mikopo yenye thamani ya shilingi za kitanzania bilioni 42 imeweza kutolewa.” Alisisitiza Bw. Ramadhani.

Kwa upande wake  Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Benki hiyo Bw. Richard Makungwa alisema benki itaendelea kuimarisha miundo mbinu yake ili kuweka mazingira mazuri ya biashara ambapo hadi hivi sasa licha ya kuwa na matawi mawili ya Dar es Salaam, Benki imefungua ofisi za kikanda zakutoa huduma katima mikoa ya Morogoro, Mwanza na Mbeya na ofisi zingine mpya Makao Makuu Dodoma na Arusha.

“Katika kuboresha utoaji huduma kupitia TEHAMA, benki ilizindua MwananchiCard VISA ambapo wateja wetu wanaweza kupata huduma kupitia ATM zaidi ya 2,000 nchi nzima, kufanya malipo kwa njia ya mtandao (Online payment) na kupitia mashine za malipo (POS-point of sales) zilizopo sehemu mbalimbali za huduma ikijumuisha maduka makubwa na mahoteli.

“Vilevile tunaboresha huduma ya MwalimuMobile (*150*31#) kwenye huduma hii na pia idadi ya MwalimuWakala imeongezeka kufikia 250.” Alifafanua Bw. Makungwa.

Alisema Benki itaendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara ili walimu binafsi wanahisa kwa ujumla kutumia huduma za Benki hiyo katika kukata bima za mali na maisha yao kupitia Benki ya Mwalimu ambayo sasa ni wakala wa bima.

kwa kufanya hivyo Wanahisa wote kwa ujumla wahamasike kutumia huduma za benki hiyo katika kufanyia shughuli zao zote za kifedha kuiwezesha Benki kujiongezea mapato ili kuharakisha muda wa kutoa gawio kwa wanahisa.

“Benki pia inategemea mapato kutoka katika miamala mbalimbali kama kutoa pesa kwenye akaunti, kutuma fedha kupitia simu vile vile kutuma pesa kwa mfumo wa kibenki (TISS/EFT) na huduma za kibenki kupitia mawakala wetu.” Alisisitiz Afisa Mkuu Mtendaji.

Aidha Bw. Makungwa alisema mipango mingine endelevu ya benki inatazamiwa kukuza amana kutoka katika ikolojia ya Elimu (education ecosystem), fedha za pensheni ya kustaafu na fedha kutoka miradi ya elimu.

Naye Katibu Mkuu wa  Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Deus Seif. Alisem, “Walimu naomba tutumie benki yetu, kuna sehemu tulizembea kidogo, wakati viongozi wetu wa Chama Cha Walimu wanaanzisha hii benki waliamini kwamba benki itakuwa na nguvu kuliko mabenki yote kwasababu waliamini walimu wasiopungua 217,000 walioko kwenye pay roll ya Januari 2015 wote watafungua akaunti na kuitumia benki yao. "Napenda niwaarifu sisi makao makuu ya CWT miamala yetu inapitia Mwalimu Commercial Bank." na sisi sote kwa umoja wetu kama tutaweza kuweka tu amana kwenye benki naamini itakuwa benki kubwa na yenye nguvu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi benki ya Walimu (Mwalimu Commercial Bank Plc), Bw.Francis C. Ramadhani (Watano kushoto) na Bodi nzima ya Wakurugenzi ya benki hiyo, wakisherehekea miaka Mitano tangu kuanzishwa kwa benki hiyo iliyokwenda sambamba na Mkutano Mkuu wa Tano wa Wanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc) jijini Arusha leo Ijumaa Oktoba 22, 2021.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Commercial Bank Plc. Bw. Francis C. Ramadhani akizungumza katika mkutano huo wa tano wa wanahisa wa benki hiyo jijini Arusha Oktoba 22, 2021
Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Deus Seif akizungumza kwenye mkutano wa tano wa wanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc. jijini Arusha Ijumaa Oktoba 22, 2021
Usajili na uhakiki wa wanahisa ukiendelea
Mkuu wa Kitengo cha Ukuzaji Biashara na Masoko wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Leticia Ndongole (kulia) akimpatia makabrasha mmoja wa wajumbe wa Mkutano huo
Wanahisa wakisikiliza yaliyokuwa yakizungumzwa na viongozi wao
Wanahisa wakiwa kwenye mkutano
Wanahisa wenye ulemavu wa kusikia, nao hawakuwa nyuma ya kikao walishiriki ipasavyo huku wakisaidiwa na mkalimani wa lugha ya alama (kulia)
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Richard Makungwa akizungumzia katika mkutano huo wa tano wa Waanahisa wa Mwalimu Commercial Bank Plc jijini Arusha Oktoba 22, 2021

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mwalimu Commercial Bank Plc. Richard Makungwa akizungumzia mafanikio ya benki katika kipindi cha miaka Mitano tangu ianzishwe.
Bodi ya Wakurugenzi Mwalimu Bank
Picha ya pamoja Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Mwalimu Bank.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...